Sunday, September 11, 2011

Makamu wa rais Dakta Mohammed Gharib Bilal atembelea Majeruhi wa Ajali ya Mv Spice Islander


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL Mama ZAKHIA BILAL na Mama ASHA BILAL, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli ya Mv SPICE ISLANDER iliyotokea eneo la Nungwi Pemba.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli, MUSSA HEMED, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.

Sunday, August 28, 2011

* Rais Jakaya Kikwete ahudhuria futari iliyoandaliwa na Makamu wake Dakta Mohammed Gharib Bila katika makazi yake OYSTERBAY Jijini Dar es Salaam


Rais Dakta JAKATA KIKWETE, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti ISSA SHAABAN SIMBA na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad MUSSA SALUM, wakisubiri muda wa swala kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Rais Dakta JAKAYA KIKWETE, Makamu wake Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, SAID MECK SADICK, wakiomba dua kwa pamoja baada ya kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais Dakta BILAL
 

Wednesday, August 24, 2011

* Viongozi wa Kitaifa wahudhuria Mazishi ya aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya Gari Mkoani Dodoma


Rais wa Zanzibar, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu MUSSA HAMIS SILIMA aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22.


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta  MOHAMMED GHARIB BILAL akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu MUSSA HAMIS SILIMA, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.



Tuesday, August 23, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein akutana na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria ya Zanzibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na uongozi wa Wizara ya katiba na Sheria, Ikulu Mjini Zanzibar katika mfululizo wa kuzungumza na kila uongozi wa wizara Visiwani humo.

Monday, August 22, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal amuaga rasmi Balozi wa Misri anayemaliza muda wake Wael Adel Nasr


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na Balozi wa Misri anayemaliza muda wake hapa nchini WAEL ADEL NASR aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga rasmi.


Makamu wa Rais wa Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL pamoja na Balozi wa Misri anayemaliza muda wake WAEL ADEL NASR aliyefika ofisini kwake Ikulu, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga, Kushoto ni Msaidizi wa Balozi huyo AMR MAHMOUD.

Sunday, August 21, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal ahudhuria Fainali za Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya pili,  Alhaj ALI HASSAN MWINYI wakiwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushirikisha jumla ya washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an JAHUDDIN ADAM kutoka Sudan mara baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj ALI HASSAN MWINYI pamoja na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Friday, August 19, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal asaini kitabu cha Makubaliano ya Mkutano wa 31 wa SADC uliofanyika mjini Luanda nchini ANGOLA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakat MOHAMMED GHARIB BILAL akisaini kitabu cha maafikiano yaliyotokana kuhusu itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu udhibiti wa fedha chafu sambamba na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama yaliyoafikiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Mataifa ya SADC mjini Luanda Angola.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, MORGAN TSVANGIRAI walipokutana kwenye mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, BERNARD MEMBE pamoja na Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Maendeleo zilizopo kusini mwa Afrika wakiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya hiyo uliomalizika nchini Angola Agosti 18, 2011.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akikagua Gwaride lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo jijini Luanda, Angola baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC