Saturday, April 21, 2012

* Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wameuwawa Jijini Dar es Salaam

DCP - SULEYMAN KOVA
Na Mwandishi
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokutwa wakiwa na silaha tatu, ambao walikuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katikati ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo DCP-SULEYMAN KOVA amesema watu hao wameuawa katika majibizano ya Risasi na Kikosi maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na Ujambazi.
Amesema kuuliwa kwa watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi kumetokana na Jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa wananchi kupitia mpango wa Polisi Jamii.
Kamanda KOVA amesema baada ya Jeshi hilo kupokea taarifa hizo walizifuatilia na kuwakuta watu hao wakiwa katika baa iliyotajwa kwa Jina la Respect mabibo wakijiandaa kwa minajili ya kwenda kutekeleaza uhalifu.
Amesema katika tukio hilo hakuna Askari wala Raia alijeruhiwa katika tukio hilo ambalo limetokea jana majira ya mchana eneo la Mburahati Madoto.

No comments:

Post a Comment