Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na wataalam wanaohusiana na sekta ya maji walipofika katika ukumbi wa mikutano wa jumuiya ya wafanya biashara, (kulia) ni Mel STEWART OBE, na PETER JACKSON,mazungumzo hayo yalifuatia baada ya makubaliano yaliyofanyika na Rais wa Zanzibar na Kiongozi wa Sharjah Sheikh Sultan MOHAMMED Al QASIMI, juu ya mashirikiano katika vyanzo vya maji safi na salama Zanzibar.
Tuesday, November 15, 2011
Sunday, November 13, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein atembelea kampuni ya Vifaa vya Ujenzi Huko Ras Al Khaimah
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akizungumza na Sheikh SAUD Bin SAQR Al QASIMI ambae ni Mwenyeji wake na Kiongozi wa Ras Al Khaimah,wakati alipowasili katika kasri ya kiongozi huyo akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano wa Ki-maendeleo katika sekta mbali mbali.
Rais wa Zanzibar Dkt ALI SHEIN akikaribishwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics, Bwana ABDALLAH MASSAAD,wakati alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya ujenzi huko Ras Al Khaimah,akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano katika sekta za maendeleo.
Rais wa Zanzibar Dkt ALI SHEIN akitembelea pamoja na kupata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics ABDALLAH MASSAAD huko Ras Al Khaimah.
Friday, November 11, 2011
* Rais Dakta Jakaya Kikwete afunga mkutano wa uwekezaji katika Sekta ya Kilimo
Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akifunga Mkutano wa Kazi uliojadili Mpango wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo mabalozi zaidi ya 15, wawakilishi wa taasisi za kimataifa, Mawaziri na Viongozi kadhaa kutoka Serikalini pamoja na wadau wa sekta ya umma.
Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akizungumza na wadau wa maendeleo baada ya kufunga Mkutano wa Kazi uliojadili Mpango wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
* Rais Dakta Jakaya Kikwete ahudhuria mkutano wa majadiliano ya Sekta Binafsi na Umma
Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akihutubia mkutano wa majadiliano ya sekta za umma-na-binafsi katika kusawazisha uwiano wa kodi kwa nchi za Afrika Mashariki ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania.
Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akiwasili katika ufunguzi wa majadilino ya sekta za umma-na-binafsi, huku akisindikizwa na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki SAMWEL SITTA.
Thursday, November 10, 2011
* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal aongoza mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa JUMANNE MAGHEMBE, akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt GHARIB BILAL, akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa JUMANNE MAGHEMBE wakati alipokuwa akiongoza Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dkt GHARIB BILAL, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na kilimo, baada ya kuongoza mkutano huo ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku mbili.
Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Balozi wa Japan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini MASAKI OKADA, alipofika Ikulu ya Mjini Zanzibar kuonana nae.
Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Japan Bwana MASAKI OKADA , alipofika ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,
* Rais Jakaya Kikwete akutana na Balozi wa Shirikisho la Urusi
Rais Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa na Balozi wa Shirikisho la Urusi ALEXANDRA RANNIKH baada ya kukutana na kuongea nae, Katikati ni mkalimani NIKITA RASSOKHIN.
Rais Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa na Balozi wa Shirikisho la Urusi Russian Federation Bwana Alexandra Alexandrovich Rannikh baada ya kukutana na kuongea nae, Ikulu jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)











