Friday, November 18, 2011

* Balozi wa kinywaji cha Hennessy awaeleza wanahabari kuhusu maajabu ya Hennessy XO


Balozi wa kinywaji cha Hennessy Bwana CYRILLE GAUTIER'S anayeishi katika ubingwa wa dunia ya maajabu ya Hennessy nchini Ufaransa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akielezea juu ya kinywaji cha Hennessy.


Balozi wa Hennessy Bwana CYRILLE GAUTIER'S akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) aina ya kinywaji cha Hennessy XO kinachotengenezwa nchini Ufaransa na kusambazwa kote Barani Afrika.

* Mke wa makamu wa Rais wa Tanzania Mama Asha Bilal ahudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi ya Alliance Francaise.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama ASHA BILAL akisoma Hotuba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam Tanzania,.iliyofanyika katika Ukumbi wa Alliance Francaise, Katikati ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini, MARCEL ESCURE,kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, JULIA GIANNETTI.


Mke wa Makamu wa Rais Mama ASHA BILAL akizungumza jambo na Balozi wa Ufaransa, MARCEL ESCURE, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Alliance Francaise.

Tuesday, November 15, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal apokea madai ya wanaharakati kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akipokea Madai ya Wananchi ya Namna ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka kwa Mwanaharakati wa Mabadiliko ya tabia Nchi LAWRENCE CHUMA wakati wa Kongamano la Msafara wa kuelekea katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi unaotarajia kufanyika Durban, Afrika Kusini mwezi ujao.


Makamu wa Rais, Dkt MOHAMMED BILAL akizungumza wakati wa Kongamano la Msafara wa kuelekea katika mkutano wa mabadfiliko ya Tabia Nchi utakaofanyika Durban, Afrika Kusini.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na wataalam wa Sekta ya Maji


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na wataalam wanaohusiana na sekta ya maji walipofika katika ukumbi wa mikutano wa jumuiya ya wafanya biashara, (kulia) ni Mel STEWART OBE, na PETER JACKSON,mazungumzo hayo yalifuatia baada ya makubaliano yaliyofanyika na Rais wa Zanzibar na Kiongozi wa Sharjah Sheikh Sultan MOHAMMED Al QASIMI, juu ya mashirikiano katika vyanzo vya maji safi na salama Zanzibar.

Sunday, November 13, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein atembelea kampuni ya Vifaa vya Ujenzi Huko Ras Al Khaimah


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akizungumza na Sheikh SAUD Bin SAQR Al QASIMI ambae ni Mwenyeji wake na Kiongozi wa Ras Al Khaimah,wakati alipowasili katika kasri ya kiongozi huyo akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano wa Ki-maendeleo katika sekta mbali mbali.


Rais wa Zanzibar  Dkt ALI SHEIN akikaribishwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics, Bwana ABDALLAH MASSAAD,wakati alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya ujenzi huko Ras Al Khaimah,akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na mashirikiano katika sekta za maendeleo.


Rais wa Zanzibar Dkt ALI  SHEIN akitembelea pamoja na kupata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ujenzi ya Rak Ceramics ABDALLAH MASSAAD huko Ras Al Khaimah.

Friday, November 11, 2011

* Rais Dakta Jakaya Kikwete afunga mkutano wa uwekezaji katika Sekta ya Kilimo


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akifunga Mkutano wa Kazi uliojadili Mpango wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo mabalozi zaidi ya 15, wawakilishi wa taasisi za kimataifa, Mawaziri na Viongozi kadhaa kutoka Serikalini pamoja na wadau wa sekta ya umma.


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akizungumza na wadau wa maendeleo baada ya kufunga Mkutano wa Kazi uliojadili Mpango wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.

* Rais Dakta Jakaya Kikwete ahudhuria mkutano wa majadiliano ya Sekta Binafsi na Umma


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akihutubia mkutano wa majadiliano ya sekta za umma-na-binafsi katika kusawazisha uwiano wa kodi kwa nchi za Afrika Mashariki ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania.


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akiwasili katika ufunguzi wa majadilino ya sekta za umma-na-binafsi, huku akisindikizwa na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki SAMWEL SITTA.