Friday, January 13, 2012

Rais Jakaya Kikwete atembelea eneo la Mabwepande na kupokea Seti ya Vyombo pamoja na taa zinazotumia nguvu ya Jua



Rais JAKAYA KIKWETE na mama SALMA KIKWETE wakioneshwa maeneo ya makazi mapya ya walioathirika na mafuriko katika bonde la Msimbazi walipotembelea eneo hilo.


Rais JAKAYA KIKWETE akipokea seti ya vyombo vya nyumbani na taa inayotumia nguvu za jua kutoka kwa Mkurugenzi wa Home Shopping Centre GHARIB SAID MOHAMMED ambaye kampuni yake imejitolea kugawa seti kama hizo pamoja na taa kwa kila familia 655 zilizohamishiwa Mabwepande baada ya kuathirika na Mafuriko katika bonge la Msimbazi, GHARIB pia ameahidi kujenga shule ya msingi ya eneo hilo pamoja na kituo cha polisi.

* Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma wameiaga miili ya wanajeshi wawili waliofariki Dunia hivi karibuni Jijini Dar es Salaam


Rais JAKAYA KIKWETE na mkewe mama SALMA KIKWETE wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Kamishna wa Magereza ELIAS MTIGE NKUKU,aliyefariki juzi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao mkoani Singida, Shughuli ya kumuaga imefanyika katika bwalo la jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.


Rais JAKAYA KIKWETE na mkewe mama SALMA KIKWETE wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Kanali PASTORY KAMUGISHA wa JWTZ aliyefariki juzi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao mkoani Kagera, Shughuli ya kumuaga marehemu imefanyika katika kambi ya jeshi ya Lugalo Jijini Dar es salaam.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein ahudhuria tamasha la Taarabu rasmi katika ukumbi wa Salama Bwawani mjini Unguja


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akiangalia taarab Rasmi iliyocharazwa na Kikundi Culture Musical Club ndani ya Ukumbi wa Salama Bwawani katika kusheherekea Miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wa kwanza kulia ni Mama Balozi SEIF ALI IDDI Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mahgaribi ABDALLAH MWINYI KHAMIS na kushoto ni Waziri wa habari Utamaduni na Michezo ABDILLAH JIHAD HASSAN.


Mwimbaji FATMA ISSA wa Kikundi cha Culture Musical Club akiwaburudisha mashabiki katika ukumbi wa Salama Bwawani kwa nyimbo ya"Umewashika" katika sherehe za Kutimiza miaka 48 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.


Wasanii wa kikundi cha muziki cha Culture Musical Club wakicharaza ala katika hafla maalum ya kusheherekea miaka 48 yaMapinduzi Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani.

Thursday, January 12, 2012

* Kamati kuu ya CCM Taifa yamchagua Mohammed Raza kuwania nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya kati Unguja

Mohammed Raza, Kada wa Siku nyingi wa chama cha Mapinduzi CCM




Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE (katikati) akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa, katika ukumbi wa chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar.

* Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yafanyika Visiwani humo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na wananchi wa Zanzibar katika kilele cha miaka 48 ya mapinduzi matukufu ya Visiwa hivyo.


Rais wa Zanzibar  Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi wakati wa Sherehe za kutimia kwa miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amaan.







Askari wa Kikosi cha JWTZ wenda kwa miguu kikipita mbele Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN na kutoa heshima kwa mwendo wa kurukaruka wakati wa sherehe za Kilele cha kutimia Miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar


Askari wa Kikosi cha Polisi FFU kikipita mbele kwa kutoa heshima ya gwaride mwendo wa pole katika kilele cha miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika jana katika uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.




Wananchi waliohudhuria katika sherehe za kutimia miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini harakati za sherehe zinavyoendelea katika uwanja wa amaan Mjini Zanzibar.


Wananchi wakishuhudia mizinga 21 ikipigwa

Monday, January 9, 2012

* Rais Jakaya Kikwete akutana na Waziri wa Uvuvi,Maliasili na Bunge wa GAMBIA, Ikulu Jijini Dar es Salaam



Rais JAKAYA KIKWETE akiwa na Waziri wa Uvuvi, Maliasili na Bunge wa Gambia na Mjumbe Maalumu wa Rais YAHYA JAMMEH, Bwana LAMIN KABA, ambaye kamletea ujumbe toka kwa Rais huyo Ikulu jijini Dar es salaam.

Saturday, January 7, 2012

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein azindua Jengo la Bodi ya Mapato la Zanzibar ZRB


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Jengo la Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB huko Mazizini Nje ya Mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 48 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akiuliza suala kwa kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar MOHAMMED HASHIM wakatiwa uzinduzi wa jengo la Bodi hiyo huko Mazizini Nje ya Mji waZanzibar.


Baadhi ya Mabalozi na Viongozi walioalikwa katika sherehe ya Uzinduzi wa Jengo la Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB hukoMazizini Nje ya Mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za miaka 48 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.