Tuesday, January 24, 2012

* Makamu wa Rais Dkt Mohammed Bilal Ziarani Mkoa wa Tanga, akagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari.


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, CHIKU GALAWA (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, MOHAMMED HAMIS.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na wizara ya kazi pamoja na Afya kwa nyakati tofauti


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ikulu Mjini Zanzibar katika mpangilio wake wa kuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.



Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji naNishati, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI SHEIN alipokuwa akizungumza na watendaji hao Ikulu Mjini Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI SHEIN alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara Afya katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar katika mpangilio wake wa kufanya mazungumzo na kila Wizara ya Serikali yake.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI SHEIN akizungumza na watendaji wa Wizara Afya, Ikulu Mjini Zanzibar ukiwa ni mpangilio wake wa kuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Thursday, January 19, 2012

* Rais Jakaya Kikwete na Dakta Mohammed Bilal waomboleza kifo cha mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari

Rais JAKAYA KIKWETE akiweka saini kitabu cha maombolezo.


 Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akiweka saini kitabu maombolezo.



Picha mbili tofauti zikiwaonesha Rais JAKAYA KIKWETE pamoja na Makamu wake Dakta MOHAMMED GHARIB bilal wakitoa Pole kwa familia ya Marehemu JEREMIAH SUMARI aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambae amefariki dunia kutokana maradhi ya kisukari.

* H-BABA akamilisha wimbo wa Sina Raha aliomshirikisha Banza Stone

Mwanamuziki H-BABA
MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis RamadhanH-Baba’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha, akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’ Mwalimu  wa Walimu.

Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar es Saam.
Pia alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe na Nimpende Nani.

* Rais Kikwete aongoza mamia katika mazishi ya Regia Mtema,Ifakara



Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Chadema marehemu REGIA MTEMA.

Wednesday, January 18, 2012

* Ujumbe wa Abort Fund wamtembelea Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na ujumbe kutoka Abort Fund, ANDY WILSON katikati na Dkt AYOUB MAGIMBA, wakati walipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam.

Tuesday, January 17, 2012

* Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chadema Marehemu Regia Mtema waagwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ZAKHIA BILAL, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu REGIA MTEMA, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu ambapo Mwili wa marehemu REGIA umeagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ZAKHIA BILAL, wakiagana na wanafamilia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu REGIA MTEMA.



Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA na mkewe Mama TUNU PINDA, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, Mwili wa marehemu REGIA umeagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.


Spika wa Bunge ANNE MAKINDA, akitoa wasifu wa marehemu katika shughuli zake za kibunge na Salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.


Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga kabla ya mwili wa Marehemu REGIA kusafirishwa kuelekea Ifakara kwa ajili ya Maziko.