Kocha wa ngumi ABDALLAH ILAMBA 'Komando' akimsimamia Bondia FRANCIS CHEKA kufanya mazoezi ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake na MADA MAUGO wa kugombea mkanda wa I.B.F pamoja na gari utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
Wednesday, April 25, 2012
Saturday, April 21, 2012
* Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wameuwawa Jijini Dar es Salaam
| DCP - SULEYMAN KOVA |
Na Mwandishi
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokutwa wakiwa na silaha tatu, ambao walikuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katikati ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo DCP-SULEYMAN KOVA amesema watu hao wameuawa katika majibizano ya Risasi na Kikosi maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na Ujambazi.
Amesema kuuliwa kwa watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi kumetokana na Jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa wananchi kupitia mpango wa Polisi Jamii.
Kamanda KOVA amesema baada ya Jeshi hilo kupokea taarifa hizo walizifuatilia na kuwakuta watu hao wakiwa katika baa iliyotajwa kwa Jina la Respect mabibo wakijiandaa kwa minajili ya kwenda kutekeleaza uhalifu.
Amesema katika tukio hilo hakuna Askari wala Raia alijeruhiwa katika tukio hilo ambalo limetokea jana majira ya mchana eneo la Mburahati Madoto.
Friday, April 20, 2012
* Rais Jakaya Kikwete amaliza Ziara ya kikazi nchini Brazil
Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa chama cha wafanya biashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo.
Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika mazungumzo na viongozi wa chama cha wafanya biashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo.
Wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa chama hicho Bwana JOAO GUILHERME na kushoto ni Mkurugenzi wa chama hicho THOMAZ ZANOTTO na kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mheshimiwa HAROUN ALI SULEIMAN.
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein azindua tanki la Maji safi wilaya ya Chake Chake Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya wananchi wa shehia ya ziwani na vijiji jirani wakimsikiliza,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN,alipokua akizungumza nao wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba.
* Viongozi wa madhehebu ya Dini wapigwa msasa kuhusu Sensa ya watu na makazi ya 2012
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi RAMADHAN KHIJJAH akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi RAMADHAN KHIJJAH alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi RAMADHAN KHIJJAH (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012.
Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. ALBINA CHUWA (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat AMINA MRISHO.
Thursday, April 19, 2012
* Mambo safi Group yaweka kambi kwa ajili ya makamuzi ya MAY DAY
Mkurugenzi wa SF GROOUP OF COMPANIES LIMITED, SELINA KOKA kushoto akimkabidhi gita kiongozi wa kundi la Mambo safi, FABBIAN SALVATORY 'Super Phabby' kwa ajili ya kuweka kambi ya siku saba ili waanze kutoa burudan kwa wakazi wa jiji ifikapo mei mosi mwaka huu.
Mkurugenzi wa SF GROOUP OF COMPANIES LIMITED, SELINA KOKA kushoto akiwa pamoja na kundi la Mambo Safi.
Na Mwandishi Wetu
KUNDI la muziki wa asili na dansi la Mambo Safi limeanza kambi rasmi leo katika ukumbi wa Harbous Klab kwa ajili ya kujiandaa na sherehe za Mei mosi zitakazofanyika katika ukumbi wa Urafiki Club, Dar es Salaam.
Kundi hilo ambalo sambamba na kutoa burudani hiyo pia linajihusisha na kucheza sarakasi pamoja na Ngonjera litakaa kambi hiyo kwa muda wa wiki moja ili kuweza kujiimarisha.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa SF group Camponies ltd ambayo ndio inasinamia kundi hilo Selina Koka alisema katika kambi hiyo watakuwa wakifanya mazoezi katika burudani zote wanazozitoa.
"kundi hili huwa linatoa burudani katika shughuli mbalimbali za kiserikali na hii ni moja ya shughuli za kiserikali na ndio maana tumeamua kuweza kambi ili kuweza kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya kusheherekea siku hiyo," alisema.
Aliongeza kuwa kundi hilo ambalo linajumla ya wanamuziki 22 linatarajia kuanza kutoa burudani kwa kila wiki katika ukumbi tofauti kama zilivyobendi nyingine ili kuweza kutoa burudani zaidi.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Phabbian Salvatory 'Super Phabby' alisema wanaliandaa kundi hilo kutoa upinzani kwa bendi nyingine kongwe kama Extra bongo, Twanga na nyinginezo ili kuweza kujiweka katika ramani nzuri ya muziki wa dansi hapa nchini.
"hatutaki kuishia hapa tunataka kuwa kama bendi nyingine na hata tuwashinde kwa kuwapa upinzani mkubwa ili kuweza kuwaonyesha uwezo wetu tulionao," alisema.

Saturday, April 14, 2012
* Tomasi Mashari amchakaza Galile kwa pointi na kunyakua Ubingwa
Bondia SELEMANI GALILE akipambanma na THOMAS MASHARI 'Simba' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa uliofanyika Dar es Salaam MASHARI alishinda kwa pointi na kunyakua ubingwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)