Saturday, March 16, 2013

* Hospitali ya KAIRUKI yatimiza miaka 25 tangu ilipoanzishwa mwaka 1987


Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya HUBERT KAIRUKI Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013


Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE, Rais Mstaafu Alhaj ALI HASSAN MWINYI, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt SALIM AHMED SALIM wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais KIKWETE alipotembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya HUBERT KAIRUKI akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.


Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mama KOKU KAIRUKI akiwa na Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji ALI HASSAN MWINYI katika Sherehe hizo.