Thursday, October 13, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal azindua kituo cha kulelea watoto yatima


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akikata utepe kuzindua rasmi Kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Full Gospel Children’s Home, kilichopo Msongola Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.




Baadhi ya watoto wakitoa burudani ya kuigiza maisha ya watoto waishio katika mazingira magumu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Full Gospel Children’s Home.

Wednesday, October 12, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein awapongeza wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 waliofanya vizuri visiwani Unguja


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na walimu na wanafunzi bora wa kidato cha nne na sita,waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2010-2011,alipokutana nao katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
 




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. ALI MOHAMMED SHEIN akipokea risala kutoka kwa mwanafunzi ALI OMAR kwa niaba ya wanafunzi bora wa kidato cha nne na sita,waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2010-2011.

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal atoa Pole kwa Familia ya Balozi Juma Mwapachu Jijini Dar es Salaam



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha HARITH MWAPACHU, ambaye ni mtoto wa Balozi JUMA MWAPACHU, aliyefariki dunia Jijini Dar es Salaam. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE, wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi JUMA MWAPACHU eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Thursday, September 29, 2011

* Shirika la Oxfam limezindua ripoti inayohusu mikataba mibovu na Uporwaji wa Ardhi Tanzania



Picha mbili tofauti zikionesha matukio yaliyojiri wakati wa uzinduzi huo ambao umefanyika katika Ofisi za OXFAM TANZANIA na kuhudhuria na wadau mbalimbali wanaojihusisha na utetezi wa migogoro ya Ardhi hapa Nchini.

Wednesday, September 21, 2011

Dakta Shein akutana kwa Nyakati tofauti na Balozi wa Japan pamoja na mwakilishi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Japan anayemaliza muda wake hapa nchini Nchini,HIROSH NAKAGAWA aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza muda wake.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na mgeni wake Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani KLAUS-PETER BRANDES aliyefika Ikulu ya mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais SHEIN.

Dakta Bilal ahudhuria Sherehe za Utiaji saini mkataba wa miradi ya makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Liganga


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa NDC na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, CHRISTANT MZINDAKAYA pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, LIU CANGLONG wakiweka saini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.

Monday, September 19, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein akutana na wananchi wa Visiwa vya Pemba na kuwapa Pole kutoka na Msiba wa ajali ya Mv Spice Islander's


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakt  ALI MOHAMMED SHEIN akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika skuli ya Piki, kuzungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaun Takao, waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv SPICE ISLANDER'S ,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliopatwa na Msiba wa jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na akizungumza na wananchi wa Daya Mtambwe wakati alipofika kuwapa Pole na kuwahutubia.




Baadhi ya wananchi wa familia zaidi ya 70 wa Kisiwa cha Piki na Mzambarun takao, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, alipofika Skuli ya Sekondari ya Piki kuwapa pole kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SPICE ISLANDER'S hivi karibuni .