Wednesday, September 21, 2011

Dakta Bilal ahudhuria Sherehe za Utiaji saini mkataba wa miradi ya makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Liganga


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa NDC na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, CHRISTANT MZINDAKAYA pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, LIU CANGLONG wakiweka saini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment