Friday, January 6, 2012

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal azindua Jengo jipya la makao makuu ya Polisi mkoa wa kusini Pemba



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akifunua Kitambaa ikiwa ni Ishara ya kuzindua rasmi Jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi lililopo eneo la Dunga, Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, MUSSA ALI MUSSA wakati akimuelekeza baadhi ya maeneo muhimu yaliyo ndani ya Jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi uliofanyika eneo la Dunga, Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Wednesday, January 4, 2012

* Rais Jakaya Kikwete aongoza mamia ya watu katika mazishi ya Balozi Athumani Mhina kijiji cha Mnyuzi, Wilayani Korogwe mkoa wa Tanga




Rais Dakta JAKAYA KIKWETE akiweka udongo katika Kaburi la Balozi ATHUMANI MHINA aliyezikwa katika kijiji cha Mnyuzi kilichopo Wilayani Korogwe.

Baadhi ya watu waliohudhuria Mazishi hayo nyumbani kwa Marehemu Balozi MHINA kijiji cha Mnyuzi wakiwa katika hali ya Majonzi na Huzuni kubwa kufuatia Msiba huo.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Balozi wa Oman na kufanya nae mazungumzo



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Oman ALI AHMED SALEH aliyefika kujitambulisha kwa Rais Ikulu Mjini Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kimemfukuza uanachama Hamad Rashid Mohammed pamoja na wenzake watatu

Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi CUF limeamua kwa wingi wa kura kumfukuza mmoja wa waasisi wa chama hicho na mwanasiasa mkongwe, mbunge wa Wawi, HAMAD RASHID MOHAMMED, pamoja na wenzake watatu.

Wanachama hao wakiongozwa na RASHID wametiwa hatiani na Baraza hilo kwa kuendesha njama za kukivuruga chama hicho.
Hamad Rashid Mohammed

Monday, January 2, 2012

*Dakta Mwinyihaji Makame akutana na wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt MWINYIHAJI MAKAME alipokuwa akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walipofika ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar ,Wabunge hao walisisitizia juu ya wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu Jumuiya hiyo na shughuli zake kwa wajumbe,kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Ughaibuni KHAMIS ALI, Mbunge Dkt SAID GHARIB BILAL na Mbunge Bi SEPTUU MOHAMMED.

* Rais Jakaya Kikwete awaapisha makatibu wakuu wawili pamoja na naibu katibu mkuu mmoja Ikulu, Jijini Dar es Salaam



Picha tatu tofauti zikiwaonesha makatibu wakuu wawili pamoja na naibu katibu mkuu mmoja ambao wameapishwa na Rais JAKAYA KIKWETE katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, SUSAN PAUL, Katibu Mkuu Ikulu, PETER ALANAMBULA ILOMO na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ELIACKIM CHACHA, kabla ya kuapishwa na Rais JAKAYA KIKWETE.


Waziri wa Nishati na Madini, WILLIAM NGELLEJA, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ELIACKIM CHACHA, baada ya kuapishwa na Rais KIKWETE Ikulu  Jijini Dar es Salaam.


Rais JAKAYA KIKWETE,akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini WILLIAM NGELLEJA na Naibu wake,ADAM MALIMA,Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo.

Sunday, January 1, 2012

* Rais Jakaya Kikwete asherehekea mkesha wa mwaka mpya 2012 katika Kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani



Rais JAKAYA KIKWETE akisalimiana na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani alipojumuika nao wanakijiji wenzake kuuaga mwaka 2011 na kuupokea mwaka 2012 kwa mkesha uliopambwa na ngoma za utamaduni na fashi fashi.



Fashi fashi ziking'arisha anga ya kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambako Rais JAKAYA KIKWETE alijumuika na wanakijiji wenzake kuuaga mwaka 2011 na kuupokea mwaka 2012 kwa mkesha uliopambwa na ngoma za utamaduni na fashi fashi.