Friday, April 13, 2012

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Mabalozi wa nchi tofauti

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Italy JAMES ALEX MSEKELA aliyefika ya Ikulu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dakta ALI SHEIN akifuatana na Balozi wa Uturuki hapa nchini ALI DAVUTOGLU aliyefika Ikulu ya mjini Zanzibar kufanya mazungumzo na Dakta SHEIN.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dakta ALI SHEIN akisalimiana na Balozi wa Burundi hapa nchini ISSA NTAMBUKA aliyefika Ikulu ya Zanzibar kuonana na Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi.

Tuesday, April 10, 2012

* Mwana-Filamu STEVEN KANUMBA azikwa Makaburi ya Kinondoni,mamia Wapoteza fahamu wakati wa Kuuaga Mwili wake


Watoto waliowahi kuigiza na marehemu STEVEN KANUMBA na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya KANUMBA.

Mama wa Marehemu STEVEN KANUMBA akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake.



Waombolezaji wa msiba wa Marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

KANUMBA atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.



Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.



Gari lililobeba mwili wa marehemu KANUMBA linaondoka katika viwanja vya Leaders kwenda Makaburi ya Kinondoni huku likiwa limezungukwa na waombolezaji.

(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)

Sunday, April 8, 2012

* Kanumba kuzikwa Makaburi ya Kinondoni Mama mzazi Atoa Msimamo

Hayati STEVEN KANUMBA
Masaa machache baada ya mama mzazi wa Kanumba kufika Jijini Dar es Salaam akitokea kwao Bukoba amekubaliana na maombi ya wapenzi wa mwanae na wana-bongo MOVIE kwamba mwanae azikwe hapa hapa DSM.

Hivyo Kanumba atazikwa makaburi ya kinondoni na ataagwa siku ya jumanne katika viwanja vya LEADERS Kinondoni.



Maneno ya Mwisho ya STEVEN CHARLES KANUMBA

* Rais Jakaya Kikwete atoa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Steven Kanumba

Rais Kikwete amefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba eneo la Sinza, Dar es Salaam, ambako amejiunga na mamia kwa mamia ya waombolezaji, wasanii na wana-familia kuombeleza kifo cha mmoja wa wasanii vijana, hodari zaidi na wenye vipaji vikubwa zaidi katika tasnia ya sanaa.

Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Kanumba, Rais Kikwete  ametia saini kitabu cha maombolezo na baadaye kuingia ndani kuzungumza kwa ufupi sana na wana-familia pamoja na wasanii wengi wa kike wa Tanzania.

Katika salamu zake za rambirambi kwa wanafamilia, Rais Kikwete amesema kwa kifupi tu: “Nimekuja kuhani msiba wa kijana wetu Steven Kanumba. Tulifahamiana sana wakati wa enzi ya uhai wake na mwaka jana nilimwalika Dodoma kwa ajili ya chakula cha mchana na wasanii wenzake wachache.

Ametutoka akiwa bado kijana sana lakini Mwenyezi Mungu ana mapenzi na uwezo wake. Nawaombeni kuweni na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba.”

Rais Kikwete pia amewaasa wasanii kuwasikiliza wana-familia katika maamuzi yote yanayohusiana na wapi azikwe marehemu. Marehemu Steven Charles Kanumba aliaga dunia usiku wa kuamkia jana, Jumamosi, Aprili 7, 2012. Alikuwa na umri wa miaka 28.

Hayati STEVEN CHARLES KANUMBA 'Mcheza Filamu'




Rais JAKAYA KIKWETE akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.



Rais KIKWETE akiongea na wanakamati ya msiba wa marehemu STEVEN KANUMBA Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam alikofika kuomboleza nao kifo hicho.

Friday, April 6, 2012

* Majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba yatangazwa




Rais JAKAYA KIKWETE akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo.

Wakishuhudia ni Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF IDDI Pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Mama CELINA KOMBANI.


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsubiri Rais KIKWETE kuja kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais KIKWETE akitoa ufafanuzi kuhusu Tume ya mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza, akisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa kwa mujibu sheria tume hiyo inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18.


   TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,

Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7

______________________________



UONGOZI WA JUU

1.Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA
- Mwenyekiti

2.Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI
- Makamu Mwenyekiti


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA

1.Prof. Mwesiga L. BAREGU


2.Nd. Riziki Shahari MNGWALI


3.Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI


4.Nd. Richard Shadrack LYIMO


5.Nd. John J. NKOLO


6.Alhaj Said EL- MAAMRY


7.Nd. Jesca Sydney MKUCHU


8.Prof. Palamagamba J. KABUDI


9.Nd. Humphrey POLEPOLE


10.Nd. Yahya MSULWA


11.Nd. Esther P. MKWIZU


12.Nd. Maria Malingumu KASHONDA


13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)


14.Nd. Mwantumu Jasmine MALALE


15.Nd. Joseph BUTIKU


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR


1.Dkt. Salim Ahmed SALIM


2.Nd. Fatma Said ALI


3.Nd. Omar Sheha MUSSA


4.Mhe. Raya Suleiman HAMAD


5.Nd. Awadh Ali SAID

6.Nd. Ussi Khamis HAJI


7.Nd. Salma MAOULIDI


8.Nd. Nassor Khamis MOHAMMED


9.Nd. Simai Mohamed SAID


10.Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA


11.Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN


12.Nd. Suleiman Omar ALI


13.Nd. Salama Kombo AHMED


14.Nd. Abubakar Mohammed ALI


15.Nd. Ally Abdullah Ally SALEH


UONGOZI WA SEKRETARIETI

1.Nd. Assaa Ahmad RASHID
- Katibu

2.Nd. Casmir Sumba KYUKI
- Naibu Katibu

Saturday, March 17, 2012

* Ujumbe wa kujitathmini Ki-Utawala Bora APRM wakutana na Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akizungumza na ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo


Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akifurahia jambo na Kiongozi wa Jopo la Wataalam kutoka Afrika wa Ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) AKERE TABENG MUNA (kulia) na Mwenyekiti wa Ujumbe huo kutoka Tanzania, HASA MLAWA (kushoto) baada kumaliza mazungumzo na Jopo hilo.


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Wajumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) baada kumaliza mazungumzo na Ujumbe huo.

Thursday, March 1, 2012

* Kocha wa Masumbwi Super D awafua Vijana wa Kambi ya Ilala



Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, RAJAB MHAMILA Super D (kulia) katika picha mbili tofauti akiwafundisha mabondia wa Kambi ya Ilala Jijini Dar es Salaam SAID MTITU pamoja na EMANNUEL MALOLO jinsi ya kutupa makonde.