Thursday, May 17, 2012

* Mafisango sasa kuagwa TCC Chang'ombe,Badala ya Viwanja vya Leaders


Marehemu PATRICK MAFISANGO


Mwili wa kiungo mahiri wa Simba Sports Club Patrick Mafisango (32), sasa utaagwa kwenye Uwanja wa TCC club, Chang'ombe, Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi badala ya Leaders Club, Kinondoni, kama ilivyotangazwa hapo awali.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geoffrey Nyange amesema kwamba wamehamishia shughuli ya kuuga mwili huo Uwanja wa Siga ratiba nyingine zote zinabaki kama ilivyotangazwa awali.

Mafisango amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.

Mafisango alifariki kutokana na ajali iliyotokea wakati gari alilokuwa akiendesha lilipogonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri ambapo Marehemu alifariki papo hapo.

Kwenye gari aliyokuwamo Mafisango, kulikuwapo na abiria wengine wanne lakini ni Mafisango pekee ndiye aliyefariki dunia.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako atazikwa.

Ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo Amavubi, Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake.

Msiba wa Mafisango uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda Sigara).

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho Ijumaa saa nne asubuhi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.

Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo, na ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume,anayeitwa Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano.

Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange na wajumbe wa kamati ya watendaji wameeleza kusikitishwa kwao na msiba huo mkubwa kwa klabu na wamewataka wana Simba wote kuwa watulivu na kumwombea marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi.

Uongozi wa Simba umeahidi kwamba utatoa taarifa nyingine zozote muhimu kwa wananchi ili wafahamu kuhusu msiba huo pale itakapotokea.



* Profesa Tibaijuka, Dakta Huvisa wapewa meno kuanza zoezi la Bomoa Bomoa Nyumba zilizojengwa maeneo ya ufukweni


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa ANNA TIBAIJUKA na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi TEREZYA HUVISA, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la bomoa bomoa ya nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni,Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam.

Katika picha kutoka (kushoto) ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt, Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt, Terezya Huvisa.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Viongozi wa wizara mbalimbali


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria, kuhusu utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar.


Viongozi wa wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dakta ALI MOHAMMED SHEIN

Sunday, May 13, 2012

Msanii wa Filamu za Kitanzania Juma Kilowoko"Sajuki" amepelekwa nchini India kwa Ajili ya Matibabu

Mwana-Filamu JUMA KILOWOKO "Sajuki" akiwa katika picha mbili tofauti, kulia ni mkewe WASTARA JUMA

Mwana-Filamu Mahiri hapa nchini JUMA KILOWOLO anayejulikana kama SAJUKI katika tasnia uigizaji,amepelekwa INDIA kwa ajili ya kufanyiwa Oparesheni ya kuondolewa uvimbe tumboni, ambapo kwa mujibu wa madaktari nchini humo wanadai kwamba upo karibu na INI.
SAJUKI ameondoka leo katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere akiambatana na mkewe WASTARA JUMA ambae pia ni Mwana-Filamu, hii ni mara ya Pili kupelekwa nchini INDIA ambapo awali alienda kwa lengo la kufanyiwa vipimo vya damu.
Kuondoka kwa SAJUKI kunafuatia Juhudi mbalimbali zilizofanywa na wasanii wa filamu pamoja wadau wengine wa tasnia hiyo wakiwemo viongozi wa juu wa Serikali.
Dua za Watanzania Bado zinahitajika kumuombea kwa mwenyezi mungu Mwana-Filamu SAJUKI ili aweze kutibiwa na kupona na hatimae arejee nchini kuendelea na majukumu yake ya Ujenzi wa Taifa……Ameein.
                                                            
                                               

Mwana - Habari Rachel Mwiligwa kuagwa katika kanisa la ANGLIKANA Ubungo


Marehemu RACHEL MWILIGWA

TANGAZO LA MSIBA
Mwili wa marehemu  RACHEL MWILIGWA aliyekuwa mhariri wa gazeti la MTANZANIA  linalomilikiwa na kampuni ya NEW HABARI CORPOROTAION  utaagwa   tarehe  14.5.2012  katika kanisa la ANGLIKANA UBUNGO jirani na Shule ya msingi ya  national housing.
Waaandishi wahabari  na wadau  wa michezo nchini wanaombwa  kujitokeza kwa wingi kuhudhuria ibada hiyo ambapo baadae saa sita mwili utapelekwa  eneo la GOBA nje  kidogo ya jiji la DSM kwa ajili ya mazishi.
Tunashukuru kwa ushirikiano ulionyeshwa   kutoka waandishi wenyewe,wananchi na wadau wa michezo nchini katika kufanikisha jambo hili.
Taarifa hii ni kwa kujubu wa kaka wa marehemu ALEX CHIMELA
Bwana ametoa  na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.

Thursday, April 26, 2012

* Mabondia Japhet Kaseba na Francis Cheka kupambana siku ya Saba saba

Bingwa Mchezo wa Kickboxing hapa nchini JAPHET KASEBA akisaini mkataba wa kupambana na FRANCIS CHEKA.


Bondia FRANCIS CHEKA akisaini mkataba wa kupambana na JAPHET KASEBA.


Na Mwandishi wetu

Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukuru kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanataka kupigana nae.



Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae.
"Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu" alisema Cheka.

"Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kiporo".

Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao haujawahi kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi
.

* Kichanga chaokotwa kitongoji cha Isevya Mkoani Tabora

Kichanga kikiwa kimetupwa na mtu ambae mpaka sasa bado hajafahamika eneo la Isevya mkoani Tabora.


Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora wakijadiliana Jambo kuhusu Tukio hilo. 

Dampo ambalo kitoto hicho kichanga kilitupwa , pembeni ni Baadhi ya wananchi pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi wakipata maelezo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.



Umati wa Wananchi wa eneo la Isevya Mkoani Tabora wakishuhudia tukio hilo la kutupwa kwa Kichanga.


Na Mwandishi wetu

Mtu asiyejulikana amekitupa kitoto kichanga kwenye dampo lililopo kwenye Soko la kata ya Isevya manispaa ya Tabora

Kichanga hicho  kinachokadiriwa kuwa na umri kati ya miezi nane na tisa kimeokotwa na mtu anayedaiwa kuwa na magonjwa ya akili ambaye alikwenda kutupa takataka katika dampo hilo na kukikuta kichanga hicho kikiwa kimefunikwa na khanga.

Hata hivyo mtu huyo anayefahamika soko la Isevya kwa kazi ya kubeba takataka,baada ya kugundua kichanga hicho kilichotapakaa damu nyingi alikichukua na kukipeleka sokoni hapo huku akilalamikia kitendo cha kutupwa kichanga hicho ambacho hakikuwa na uhai.

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Isevya walistaajabu tukio hilo huku zikiwashangaza zaidi kauli za mtu huyo ambaye huwa wakimfahamu kwa mapungufu ya akili.

Kwa upande mwingine maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho huku wakiwaomba wananchi kutoa taarifa za mtu atakayebainika kuwa amehusika na tukio hilo la kinyama.
 
Hata hivyo katika kata ya Isevya matukio utoaji mimba na kutupa watoto yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ingawa mara nyingi wanaojihusisha na matendo hayo wamekuwa wakifichwa.