Wednesday, May 23, 2012

* Msondo Ngoma kupagawisha wapenzi wake Ndani ya Masasi


Rajabu Mhamila - Msemaji wa Bendi ya Msondo


Baadhi ya Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma

Na : Mwandishi wetu

BENDI Kongwe ya Msondo ngoma ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa wa kisasa wa burudani  wa Emirate Hall uliopo Masasi June 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani

"Unajua sisi ni baba ya Muziki nchini ndio mana wapenzi wengi wanaitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo tutatoa burudani ya uwakika" alisema

Siku hiyo tutapiga vibao vetu vya zamani na vipya kwa sasa alivitaja baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo vile vile watapiga nyimbo zao za zamani zilizotamba wakati huo.

Alisema Super D Kundi hilo litaambatana na wanamziki wake wote wakiwemo wakongwe katika mziki wa Dansi Nchini Maalimu Gulumo ' Kamana' Saidi Mabela ' DKT Mabela' na wengine wote watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wao wa Masasi Aliongeza Super D. 

* Mama Asha Bilal Mgeni Rasmi maadhimisho ya miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama ASHA BILAL, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.



Mchezaji wa mpira wa Kikapu HASHEEM THABEET, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo  wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation.


Mke wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mama MARGARETH SITTA, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Thursday, May 17, 2012

* Mafisango sasa kuagwa TCC Chang'ombe,Badala ya Viwanja vya Leaders


Marehemu PATRICK MAFISANGO


Mwili wa kiungo mahiri wa Simba Sports Club Patrick Mafisango (32), sasa utaagwa kwenye Uwanja wa TCC club, Chang'ombe, Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi badala ya Leaders Club, Kinondoni, kama ilivyotangazwa hapo awali.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geoffrey Nyange amesema kwamba wamehamishia shughuli ya kuuga mwili huo Uwanja wa Siga ratiba nyingine zote zinabaki kama ilivyotangazwa awali.

Mafisango amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.

Mafisango alifariki kutokana na ajali iliyotokea wakati gari alilokuwa akiendesha lilipogonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri ambapo Marehemu alifariki papo hapo.

Kwenye gari aliyokuwamo Mafisango, kulikuwapo na abiria wengine wanne lakini ni Mafisango pekee ndiye aliyefariki dunia.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako atazikwa.

Ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo Amavubi, Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake.

Msiba wa Mafisango uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda Sigara).

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho Ijumaa saa nne asubuhi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.

Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo, na ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume,anayeitwa Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano.

Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange na wajumbe wa kamati ya watendaji wameeleza kusikitishwa kwao na msiba huo mkubwa kwa klabu na wamewataka wana Simba wote kuwa watulivu na kumwombea marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi.

Uongozi wa Simba umeahidi kwamba utatoa taarifa nyingine zozote muhimu kwa wananchi ili wafahamu kuhusu msiba huo pale itakapotokea.



* Profesa Tibaijuka, Dakta Huvisa wapewa meno kuanza zoezi la Bomoa Bomoa Nyumba zilizojengwa maeneo ya ufukweni


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa ANNA TIBAIJUKA na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bi TEREZYA HUVISA, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la bomoa bomoa ya nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni,Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam.

Katika picha kutoka (kushoto) ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt, Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt, Terezya Huvisa.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Viongozi wa wizara mbalimbali


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria, kuhusu utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar.


Viongozi wa wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dakta ALI MOHAMMED SHEIN

Sunday, May 13, 2012

Msanii wa Filamu za Kitanzania Juma Kilowoko"Sajuki" amepelekwa nchini India kwa Ajili ya Matibabu

Mwana-Filamu JUMA KILOWOKO "Sajuki" akiwa katika picha mbili tofauti, kulia ni mkewe WASTARA JUMA

Mwana-Filamu Mahiri hapa nchini JUMA KILOWOLO anayejulikana kama SAJUKI katika tasnia uigizaji,amepelekwa INDIA kwa ajili ya kufanyiwa Oparesheni ya kuondolewa uvimbe tumboni, ambapo kwa mujibu wa madaktari nchini humo wanadai kwamba upo karibu na INI.
SAJUKI ameondoka leo katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere akiambatana na mkewe WASTARA JUMA ambae pia ni Mwana-Filamu, hii ni mara ya Pili kupelekwa nchini INDIA ambapo awali alienda kwa lengo la kufanyiwa vipimo vya damu.
Kuondoka kwa SAJUKI kunafuatia Juhudi mbalimbali zilizofanywa na wasanii wa filamu pamoja wadau wengine wa tasnia hiyo wakiwemo viongozi wa juu wa Serikali.
Dua za Watanzania Bado zinahitajika kumuombea kwa mwenyezi mungu Mwana-Filamu SAJUKI ili aweze kutibiwa na kupona na hatimae arejee nchini kuendelea na majukumu yake ya Ujenzi wa Taifa……Ameein.
                                                            
                                               

Mwana - Habari Rachel Mwiligwa kuagwa katika kanisa la ANGLIKANA Ubungo


Marehemu RACHEL MWILIGWA

TANGAZO LA MSIBA
Mwili wa marehemu  RACHEL MWILIGWA aliyekuwa mhariri wa gazeti la MTANZANIA  linalomilikiwa na kampuni ya NEW HABARI CORPOROTAION  utaagwa   tarehe  14.5.2012  katika kanisa la ANGLIKANA UBUNGO jirani na Shule ya msingi ya  national housing.
Waaandishi wahabari  na wadau  wa michezo nchini wanaombwa  kujitokeza kwa wingi kuhudhuria ibada hiyo ambapo baadae saa sita mwili utapelekwa  eneo la GOBA nje  kidogo ya jiji la DSM kwa ajili ya mazishi.
Tunashukuru kwa ushirikiano ulionyeshwa   kutoka waandishi wenyewe,wananchi na wadau wa michezo nchini katika kufanikisha jambo hili.
Taarifa hii ni kwa kujubu wa kaka wa marehemu ALEX CHIMELA
Bwana ametoa  na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.