Thursday, November 10, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal aongoza mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa JUMANNE MAGHEMBE, akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt GHARIB BILAL, akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa JUMANNE MAGHEMBE wakati alipokuwa akiongoza Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo ambao umefanyika  Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais, Dkt GHARIB BILAL, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na kilimo, baada ya kuongoza mkutano huo ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku mbili.

Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Balozi wa Japan


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini MASAKI OKADA, alipofika  Ikulu ya Mjini Zanzibar kuonana nae.


Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Japan Bwana MASAKI OKADA , alipofika ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,

* Rais Jakaya Kikwete akutana na Balozi wa Shirikisho la Urusi


Rais Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa na Balozi wa Shirikisho la Urusi ALEXANDRA RANNIKH baada ya kukutana na kuongea nae, Katikati ni mkalimani NIKITA RASSOKHIN.


Rais Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa na Balozi wa Shirikisho la Urusi Russian Federation Bwana Alexandra Alexandrovich Rannikh baada ya kukutana na kuongea nae, Ikulu jijini Dar es salaam.

Wednesday, October 26, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Balozi wa Finland Sinikka Antila katika Ikulu ya Mjini Zaznibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Finland nchini Tanzania, SINIKKA ANTILA ,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.

* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal ahudhuria na kutembelea Banda la Tanzania wakati wa mkutano wa Kimataifa wa mawasiliano ITU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa ITU uliofanyika Geneva Switzelrand.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) PETER MASIKA kuhusu namna ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta, wakati akikagua banda la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) ambao umefanyika Geneva, Switzerland.

Monday, October 24, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein aapishwa na kuwa mjumbe wa kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN  akipokea hati ya kiapo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN baada ya kuapa kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu namba 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wote.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALl MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE mara baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tuesday, October 18, 2011

* Ajali ya moto yateketeza maduka manne Singida mjini




Picha mbili tofauti zikionesha tukio la moto pamoja na jitihada za kikosi cha zimamoto katika kukabiliana na moto huo ili usisambae kwenda katika maduka mengine.