Monday, October 24, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein aapishwa na kuwa mjumbe wa kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN  akipokea hati ya kiapo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN baada ya kuapa kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu namba 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wote.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALl MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE mara baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment