Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akiangalia maonesho ya bidhaa mbali mbali za vikundi vya ushirika vya akinamama,katika viwanja vya Salama Bwawani Hoteli,ikiwa ni njia moja ya kuvitangaza vikundi hivi katika mkutano wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliomalizika jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akipata maelezo kutoka kwa SAIDA ALI MOHAMMED wa Wizara ya Ustawi wa Jamii maendeleo ya wanawake na watoto wakati alipotembelea maonesho ya bidhaa mbali mbali za vikundi vya ushirika vya akinamama.
Rais wa Shirika la African Investiment Corporation ambae pia mtendaji mkuu kutoka Marekani Daniel Anagho akitoa mada inayohusu Masuala ya utalii katika mkutano wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliomalizika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment