Picha mbili tofauti zikionesha matukio yaliyojiri wakati wa uzinduzi huo ambao umefanyika katika Ofisi za OXFAM TANZANIA na kuhudhuria na wadau mbalimbali wanaojihusisha na utetezi wa migogoro ya Ardhi hapa Nchini.
Thursday, September 29, 2011
Wednesday, September 21, 2011
Dakta Shein akutana kwa Nyakati tofauti na Balozi wa Japan pamoja na mwakilishi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Japan anayemaliza muda wake hapa nchini Nchini,HIROSH NAKAGAWA aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza muda wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na mgeni wake Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani KLAUS-PETER BRANDES aliyefika Ikulu ya mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais SHEIN.
Dakta Bilal ahudhuria Sherehe za Utiaji saini mkataba wa miradi ya makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Liganga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa NDC na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, CHRISTANT MZINDAKAYA pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, LIU CANGLONG wakiweka saini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.
Monday, September 19, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein akutana na wananchi wa Visiwa vya Pemba na kuwapa Pole kutoka na Msiba wa ajali ya Mv Spice Islander's
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakt ALI MOHAMMED SHEIN akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika skuli ya Piki, kuzungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaun Takao, waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv SPICE ISLANDER'S ,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliopatwa na Msiba wa jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na akizungumza na wananchi wa Daya Mtambwe wakati alipofika kuwapa Pole na kuwahutubia.
Baadhi ya wananchi wa familia zaidi ya 70 wa Kisiwa cha Piki na Mzambarun takao, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, alipofika Skuli ya Sekondari ya Piki kuwapa pole kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SPICE ISLANDER'S hivi karibuni .
Friday, September 16, 2011
Kundi la Muziki wa taarabu la T-Moto limesogeza mbele uzinduzi wa albamu yake ili kuomboleza msiba wa meli ya Mv Spice Islander's
Kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) limesogeza mbele uzinduzi wake uliokuwa ufanyike Septemba 30 mwaka huu hadi Oktoba 28.
Kundi hilo lililoondoka jijini na kuweka kambi ya maandalizi katika Visiwa vya Zanzibar hivi karibuni limeamua kusimamisha mazoezi yake kwa muda wa wiki moja na nusu kufuatia msiba mkubwa ulioikumba nchi kutokana na ajali ya meli ya Mv SPICE ISLANDER'S iliyozama eneo la Nungwi hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu wengi na majeruhi ikiwa ni idadi ambayo haijawahi kutokea ndani ya Visiwa hivyo.
Mkurugenzi wa kundi hilo, AMIN SALMIN ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, SALMIN AMOUR ‘Komandoo’, amesema kutokana na kundi hilo kutambua ukubwa wa msiba huo ulio na idadi kubwa ya vifo vya watu kulinganisha na idadi ndogo ya watu waishio visiwani humo, wameamua kusitisha kambi ya mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya kundi hilo kuwa katika maombolezo.
Amesema kuwa wasanii wa kundi hilo wataendelea kubaki kambini bila kuendelea na mazoezi hayo ya maandalizi ya uzinduzi wao, hadi baada ya wiki moja na nusu kuanzia siku ya kwanza kati ya tatu za maombolezo zilizotangazwa na Serikali ya Zanzibar.
Kundi hilo linatarajia kuwasili jijini wiki ijayo kwa ajili ya kuingia studio kurekodi nyimbo zake mbili zilizokwisha kamilika na kurejea tena Zanzibar kuendelea na kambi hiyo
Thursday, September 15, 2011
Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Etisalat yakutana na Dakta Shein Ikulu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Uongozi wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Etisalat, walipofika Ikulu mjini zanzibar kumpa pole Rais, kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SPICE ISLANDERS, iliyokuwa ikielekea kisiwani Pemba.
Rais wa Visiwa vya Comoro Dakta IKILILOU DHOININE awasili nchini
Rais wa Visiwa vya Comoro Dakta IKHILILOU DHOININE amewasili nchini leo mchana akiwa ameambatana na ujumbe wake na kupokewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maofisa wa Comoro zimeeleza kwamba lengo la ziara ya Dakta DHOININE ni kutoa pole kwa rais KIKWETE kutokana na vifo vya wananchi vilivyotokana na ajali ya meli ya Mv SPICE ISLANDER iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba.
Wednesday, September 14, 2011
Ujumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM watoa Pole kwa rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara PIUS MSEKWA akiongoza ujumbe wa CCM uliofika Ikulu Mjini Zanzibar,kumpa pole kutokana na Msiba kwa wananchi,waliofariki kwa ajali ya Meli ya Mv SPICE ISLANDER ambayo ilizama Ijumaa ya wiki iliyopita huko Bahari ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ilipokuwa ikielekea Pemba.
Makamu wa rais Dakta Mohammed Gharib Bilal ahudhuria Maonesho ya Miaka 35 ya Utendaji kazi wa reli ya Tazara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Balozi wa Zambia hapa nchini MAVIS LENGALENGA (kushoto) akicheza ngoma ya asili iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha Sanaa cha Makanjani kutoka Zambia, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, Maonyesho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Sunday, September 11, 2011
Idadi ya waliofariki katika ajali Mv Spice Islander yafikia 240,huku jitihada ya uokoji wa manusura na miili zikiendelea eneo la Nungwi visiwani Zanzibar.
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU pamoja na wanaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv SPICE ISLANDER,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja.
Makamu wa rais Dakta Mohammed Gharib Bilal atembelea Majeruhi wa Ajali ya Mv Spice Islander
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL Mama ZAKHIA BILAL na Mama ASHA BILAL, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli ya Mv SPICE ISLANDER iliyotokea eneo la Nungwi Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli, MUSSA HEMED, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Subscribe to:
Posts (Atom)