Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt MWINYIHAJI MAKAME alipokuwa akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walipofika ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar ,Wabunge hao walisisitizia juu ya wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu Jumuiya hiyo na shughuli zake kwa wajumbe,kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Ughaibuni KHAMIS ALI, Mbunge Dkt SAID GHARIB BILAL na Mbunge Bi SEPTUU MOHAMMED.
Monday, January 2, 2012
* Rais Jakaya Kikwete awaapisha makatibu wakuu wawili pamoja na naibu katibu mkuu mmoja Ikulu, Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, WILLIAM NGELLEJA, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ELIACKIM CHACHA, baada ya kuapishwa na Rais KIKWETE Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais JAKAYA KIKWETE,akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini WILLIAM NGELLEJA na Naibu wake,ADAM MALIMA,Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo.
Sunday, January 1, 2012
* Rais Jakaya Kikwete asherehekea mkesha wa mwaka mpya 2012 katika Kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais JAKAYA KIKWETE akisalimiana na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani alipojumuika nao wanakijiji wenzake kuuaga mwaka 2011 na kuupokea mwaka 2012 kwa mkesha uliopambwa na ngoma za utamaduni na fashi fashi.
Fashi fashi ziking'arisha anga ya kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambako Rais JAKAYA KIKWETE alijumuika na wanakijiji wenzake kuuaga mwaka 2011 na kuupokea mwaka 2012 kwa mkesha uliopambwa na ngoma za utamaduni na fashi fashi.
Saturday, December 31, 2011
* Rais Jakaya Kikwete amuapisha Balozi Ombeni Yohana kuwa katibu mkuu kiongozi Mpya
Rais JAKAYA KIKWETE, akimuapisha rasmi Balozi OMBENI YOHANA SEFUE kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, aliyemaliza muda wake.
Rais JAKAYA KIKWETE, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL,Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA na Balozi Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, mara baada ya kuapishwa na Rais KIKWETE kuwa katibu mkuu kiongozi mpya.
Rais JAKAYA KIKWETE, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein atoa Salamu za Mwaka mpya kwa Watanzania
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akitoa salamu za kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 Biladiya, kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kuwatakia amani na utulivu, ambapo amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali yao kwa michango mbali mbali katika jitihada za kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.
Friday, December 30, 2011
* Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC John Ngahyoma afariki Dunia Jijini Dar es Salaam
![]() |
| Marehemu JOHN NGAHYOMA enzi ya Uhai wake |
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ya Uingereza, JOHN NGAHYOMA amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake eneo la Segerea Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Familia ya NGAHYOMA imesema kwamba Marehemu JOHN alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kansa katika ini iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu, ambapo amewahi kwenda kutibiwa mara mbili nchini INDIA.
Marehemu NGAHYOMA anatazamiwa kuzikwa siku ya Jumapili katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
* Rais Jakaya Kikwete atoa Heshima za Mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji wa TBC, Halima Mchuka
![]() |
Rais JAKAYA KIKWETE na waombolezaji wakiombea mwili wa HALIMA MCHUKA |
![]() |
| Aliyekuwa mtangazaji wa TBC Hayati Bi HALIMA MCHUKA |
![]() |
Rais JAKAYA KIKWETE akiwapa pole wafiwa |
Subscribe to:
Posts (Atom)






















