Friday, July 6, 2012

* Rais Jakaya Kikwete aongoza Baraza la Mawaziri pamoja na Viongozi wa Serikali Mjini Dodoma


Rais JAKAYA KIKWETE akiongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akimwakilisha Rais JAKAYA KIKWETE, kuongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri, kilichofanyika katika Ukumbi wa Tamisemi Mjini Dodoma.


Rais JAKAYA KIKWETE akiongea Jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi Serikalini  baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma.

Tuesday, July 3, 2012

* Rais Jakaya Kikwete arejea nchini akitokea Burundi na Rwanda alikohudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa nchi Hizo


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE na Mama SALMA KIKWETE wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Burundi na Rwanda walikohudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo.
 
Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAID MECKY SADIK.
 
 

Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande SAID MWEMA na Mkuu wa Majeshi Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Burundi na Rwanda walikohudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo.

* Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Lugalo ya Jijini DSM, watembelea Bungeni Mjini Dodoma


Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao, nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, wakati walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge, wakiwa katika ziara yao ya Kimasomo.







Miongoni mwa wanafunzi hawa, wapo Walimu, Mawaziri, Makatibu, Madaktari, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa miaka ijayo, endapo watapewa misingi ya elimu iliyo bora na kupewa elimu ya Nidhamu na utiifu wakiwa bado wadogo, ili waje kuwa viongozi bora siku za baadaye.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein aelekea nchini Uingereza kwa Ziara Maalum


Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais Balozi SEIF ALI IDDI pamoja na viongozi wengine katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akielekea Nchini Uingereza kwa Ziara maalum, katika safari hiyo Dk SHEIN amefuatana na Mkewe Mama MWANA MWEMA SHEIN.     

Friday, June 29, 2012

* Kampuni ya Simu ya tiGO yaendeleza Shangwe kwa Wateja wake Mjini Kahama





 
Picha mbalimbali zinazoonyesha matukio tofauti yaliyofanyika wakati wa tamasha la Tigo lililofanyika Mjini Kahama katika eneo la stendi ndogo, katika tamasha hilo burudani zilitolewa na kikundi cha sarakasi na msanii H. Baba kutoka mjini Dar es Salaam aliwapagawisha kwa Burudani safi ya Muziki wateja wa Kampuni hiyo.

Pia wateja wa Tigo walipata fursa ya kushinda zawadi mbalimbali kama vile simu, Tshirt na kofia za TigoVilevile huduma za Tigo zilipatikana katika viwanja hivyo.

* tiGO yamkabidhi hundi ya Shillingi milioni Mshindi wa Promosheni inayoendelea ya Tigo-Beatz Bi Zumra Mohammed


Tigo Public Relations Officer, Ms ALICE MARO (left) hands over a dummy cheque of Sh 10,000,000 to Ms ZUMRA MOHAMMED during a press conference held in Moshi.

Ms MOHAMMED was selected randomly during a live draw last week as the first winner of  the on-going Tigo Beatz promotion.

Standing in the centre is Mr ABUBAKARI MASSOLI, Tigo Customer Service and Sales Representative, Kilimanjaro. Far right is Mr MOHAMMED HASSAN RAJAB, Administrative, Kilimanjaro.


Ms ZUMRA MOHAMMED, the first winner of the on-going Tigo Beatz promotion, proudly holds up a dummy cheque of Sh 10,000,000 from Tigo.

Thursday, June 14, 2012

* Waziri wa Habari Azungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Jijini Mwanza


Waziri wa Habari vijana, Utamaduni na Michezo Dakta FENELLA MUKANGARA akiongea na maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali jijini Mwanza.

Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na serikali kupitia vyombo vya habari.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo SETH KAMUHANDA mstari wa kwanza) akifuatilia mada  kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia  kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali ijini Mwanza.

Wengine wanaoonekana kwa nyuma ni maafisa habari na mawasiliano wa Serikali.


Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ijini Mwanza.