Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao, nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, wakati walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge, wakiwa katika ziara yao ya Kimasomo.
Miongoni mwa wanafunzi hawa, wapo Walimu, Mawaziri, Makatibu, Madaktari, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa miaka ijayo, endapo watapewa misingi ya elimu iliyo bora na kupewa elimu ya Nidhamu na utiifu wakiwa bado wadogo, ili waje kuwa viongozi bora siku za baadaye.
No comments:
Post a Comment