Wednesday, November 30, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal afunga mkutano wa nchi za maziwa makuu mjini Bujumbura


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt JAMES MWASI baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu.


Waziri wa Afrika Mashariki, SAMUEL SITTA akiwa katika Ukumbi wa Golf akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL alipokuwa akifunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliomalizika mjini Bujumbura nchini Burundi.

Monday, November 28, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal afungua Mkutano wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga CHIKU GALAWA na waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, MATHIAS CHIKAWE.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA mara baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa Viongozi wa Takukuru.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru, uliofanyika Mkoani Tanga Kushoto ni waziri wa Ofisi ya Rais- Utawala Bora, MATHIAS CHIKAWE.


Baadhi ya Wakuu wa Vitengo wa Takukuru waliohudhuria Mkutano huo Mkuu wa Mwaka ulioanza leo Novemba 28 na kumalizika kesho, Mkoani Tanga.

Saturday, November 26, 2011

* Mwakilishi wa UNDP amaliza muda wake wa kazi hapa nchini


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na mwakilishi wa Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP anayeishi Visiwani humo, SORO KARNA aliyefika Ikulu ya Mjini Zanzibar kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi hapa nchini.

Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na mwakilishi wa UNDP Bwana SORO KARNA aliyefika Ikulu ya Mjini Zanzibar kumuaga Rais.

* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal azindua Tamasha la utamaduni wa Mtanzania


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa baada ya uzinduzi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania ndani ya kijiji cha Makumbusho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimsikiliza Waziri Mkuu MIZENGO PINDA wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimshuhudia Waziri Mkuu MIZENGO PINDA akinywa kinywaji cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

* Mahafali ya Pili ya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM yafana


Kiongozi wa timu ya Viongozi wa Juu wa UDOM wakiwa katika Maandamano ya kuelekea kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.


Baadhi ya Viongozi chuo kikuu cha Dodoma wakiwa tayari kwenye Maandamano kuelekea kwenye Mahafali ya Pili ya chuo hicho.


Viongozi wa chuo kikuu cha Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa chuo hicho Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BENJAMIN WILLIAM MKAPA wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa unaimbwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM


Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sosholojia wakiwa katika furaha Mara baada ya kutunukiwa Shahada zao.

Friday, November 25, 2011

* Kampuni ya Tigo Tanzania yakabidhi Majengo ya madarasa mawili kwa Shule ya Msingi ya Pugu kajiungeni


Mwakilishi wa kampuni ya Tigo ALEX MSIGARA akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni wakati wa kukabidhi madarasa jijini Dar es Salaam, Kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. MARIAM KORONGO, kushoto kwake ni Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu (W) Ilala ABILAH MCHIA.


Afisa Elimu, ABILAH MCHIA akizungumza na waandishi wa habari na walimu wakati kampuni ya Tigo ilipokuwa ikikabidhi  madarasa mawili ya Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni jijini Dar Es Salaam, Kulia kwake ni mwakilishi wa Tigo ALEX MSIGARA na mwalimu mkuu Bi. MARIAM KORONGO.


Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, ALEX MSIGARA akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni Bi MARIAM KORONGO madaftari, kalamu za Tigo pamoja na T-shirt.

Tigo yakabidhi madarasa mawili

Tarehe 22 November 2011, Dar es Salaam, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo  imekabidhi madarasa mawili kwa shule ya msingi Pugu Kajiungeni iliyopo eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam baada ya kumaliza ukarabati wa majengo ya shule hiyo yaliyoharibiwa na mlipuko wa mabomu yaliyolipuka katika kambi ya Gongolamboto mwezi May jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabithi rasmi majengo hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Afisa viwango na mwakilishi wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Alex Msigara amesema “Sisi kama kampuni ya simu za mikononi ya Tigo tuliguswa kwa namna ya kipekee na tukio hili hasa ukichukulia kuwa wahanga wakubwa walikuwa ni watoto ambao walitaharuki na kuanza kukimbia huku na huko, na wengine kushindwa kwenda shule kutokana na mjengo kuharibika hali iliyowaondolea amani wakiwa shule”

Alex akaongeza “Nadhani waandishi na wananchi wanaoipenda Tigo watakuwa ni mashahidi kuwa sisi tumekuwa mstari wa mbele katika kuchangia elimu hasa elimu ya msingi ambapo tumeweza kutoa vitabu na vibao vya mapajani siku chache zilizopita kwa baadi ya shule za msingi nchini kwani tunaamini watoto wakikua katika misingi yenye yenye uelekeo mzuri kielimu basi wao ndio watakaoijenga Tanzania nzuri siku za usoni”

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni Bi Mariam Korongo akitoa shukrani zake kwa Tigo amesema “kwa niaba ya walimu, wazazi wa wanafunzi na wanafunzi wenyewe wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa msaada huu wa kutengenezewa madarasa haya mawili. Tunashukuru kuona kwamba taasisi binafsi zinakuwa zinaguswa na matatizo yanayozikumba jamii inayozizunguka kwani hiyo inapunguza mzigo kwa serikali ambayo inafanya juhudi kubwa katika kuhakikisha inaleta maendeleo nchini.”

Mwalimu mkuu akaongeza pia kuwa anafurahi kwamba Tigo wameweza kuwasaidia katika tatizo hilo la ukarabati wa majengo na kuziomba taasisi nyingine kuchangia sekta ya elimu katika shule mbalimbali kwani matatizo yanafanana nchini kote.

Mara baada ya tukio la mlipuko wa mabomu familia za maeneo yale zilipata misukosuko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupotezana kwa hofu, kuharibika kwa makazi na maeneo ya biashara, Tigo ilitembelea maeneo yale na kujionea jinsi uharibifu ulivyotokea na kuwapa mkono wa pole wahanga na namna ya pekee ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu la kukarabati majengo ya shule yaliyoharibiwa.

Tuesday, November 22, 2011

Kikao cha kamati kuu CC ya chama cha Mapinduzi CCM kinaendelea Mjini Dodoma



Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa wa chama hicho wakisubiri kuanza kwa kikao ambacho kinaingia siku ya pili mjini Dodoma.