Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa baada ya uzinduzi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania ndani ya kijiji cha Makumbusho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimsikiliza Waziri Mkuu MIZENGO PINDA wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimshuhudia Waziri Mkuu MIZENGO PINDA akinywa kinywaji cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment