Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, JAMES MUCHIRI (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mikopo wa benki hiyo Bi REGINA MWENGI , PRISCILLA KAROBIA na DAVID MUTHUNGU kabla ya kuanza kwa michuano ya gofu iliyoandaliwa na Lions Club na kufanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
PRISCILLA KAROBIA ambaye ni mmoja ya wanachama wa Klabu ya Gymkhana akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona.
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, JAMES MUCHIRI akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona ambapo benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NIC Tanzania akiwemo Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, JAMES MUCHIRI (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama Lions Club wakati wa michuano ya Gofu iliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho.
Benki NIC Tanzania yajitosa kudhamini Gofu kusaidia wenye uoni hafifu
Benki ya NIC Tanzania kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Jijini Dar es Salaam wamejitokeza kudhamini mashindano ya mchezo ya Gofu ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho.
Katika mashindano hayo benki hiyo imetoa jumla ya Dola za Kimarekani 2000 sawa na Shilingi Milioni 3.5 za Tanzania lengo likiwa ni kuinua afya za wananchi hususani wanaosumbuliwa na matatizo ya macho.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 105, Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa NIC Bank Tanzania James Muchiri amesema ni matarajio yao kwamba udhamini huo utasaidia upatikanaji wa afya bora katika eneo wanalotoa huduma zake.
“Tunatarajia msaada huu ambao ni wa kwanza katika sekta hii ya michezo kupitia Lions Club utasaidia watu wenye matatizo wa macho katika maeneo watakayoenda kutoa huduma hiyo kama ilivyo kawaida ya wana Mzizima,” alisema Muchiri.
Mbali na hayo Mkurugenzi na Mtendaji huyo Mkuu wa NIC Bank Tanzania alisema inakadiwa kuwa zaidi ya watu milioni tatu nchini wanakabiliwa na upofu kutyokana na uwezo mdogo wa kifedha, miongoni mwao wakiwemo wanafunzi.
Kutokana na hilo alisema watahakikisha wanajenga uhusiano mzuri baina yao na Lions Club katika kuunga mkono mchezo wa gofu na kuwahudumia wenye matatizo ya macho.
Nchini Benki hiyo ina matawi Harbour View Tower jijini Dar es Salaam, Mwanza and Arusha huku ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.
No comments:
Post a Comment