Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam MECKY SADICK (kulia) wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo eneo la Jangwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na Bi MONICA LUIS Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi.
No comments:
Post a Comment