Saturday, July 28, 2012

* Rais Jakaya Kikwete afungua Kongamano la Uhusiano baina ya Afrika na China



Rais JAKAYA KIKWETE akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini.

Wa tatu kutoka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini FAN XIAOJIAN, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais STEVEN WASSIRA, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone MOMODU KARGBO, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dakta PHILLIP MPANGO na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini L.V. YOUQING.


Rais JAKAYA KIKWETE akimsikiliza  Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini FAN XIAOJIAN (kushoto) na  Balozi wa China hapa nchini L.V. YOUQING, baada ya kufungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini.


Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe toka China wanaohudhuria Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini.

Friday, July 6, 2012

* Rais Jakaya Kikwete aongoza Baraza la Mawaziri pamoja na Viongozi wa Serikali Mjini Dodoma


Rais JAKAYA KIKWETE akiongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akimwakilisha Rais JAKAYA KIKWETE, kuongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri, kilichofanyika katika Ukumbi wa Tamisemi Mjini Dodoma.


Rais JAKAYA KIKWETE akiongea Jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi Serikalini  baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma.

Tuesday, July 3, 2012

* Rais Jakaya Kikwete arejea nchini akitokea Burundi na Rwanda alikohudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa nchi Hizo


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE na Mama SALMA KIKWETE wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Burundi na Rwanda walikohudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo.
 
Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAID MECKY SADIK.
 
 

Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande SAID MWEMA na Mkuu wa Majeshi Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Burundi na Rwanda walikohudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo.

* Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Lugalo ya Jijini DSM, watembelea Bungeni Mjini Dodoma


Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao, nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, wakati walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge, wakiwa katika ziara yao ya Kimasomo.







Miongoni mwa wanafunzi hawa, wapo Walimu, Mawaziri, Makatibu, Madaktari, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa miaka ijayo, endapo watapewa misingi ya elimu iliyo bora na kupewa elimu ya Nidhamu na utiifu wakiwa bado wadogo, ili waje kuwa viongozi bora siku za baadaye.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein aelekea nchini Uingereza kwa Ziara Maalum


Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais Balozi SEIF ALI IDDI pamoja na viongozi wengine katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akielekea Nchini Uingereza kwa Ziara maalum, katika safari hiyo Dk SHEIN amefuatana na Mkewe Mama MWANA MWEMA SHEIN.