Rais wa Zabziar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii ,Utamaduni na Michezo, katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, Ikiwa ni mfululizo wa ratiba zake za kuzungumza na kila Wizara,katika kuhakikisha taasisi za wizara hizo zinatekeleza majukumu yake.
Wednesday, August 17, 2011
Tuesday, August 16, 2011
* Wananchi wa Vijiji vitano katika wilaya ya Bagamoyo kufaidika na mradi wa visima
Kutoka kushoto ni BERTHA IKUA wa kampuni ya Spear head Africa Dakta SALIM ABDULLA Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara pamoja na NARCISIUS NGAILLO ambae ni meneja mauzo wa kampuni ya Vinywaji ya Tanzania Distillers Limited wakizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa mradi wa uchimbaji wa Visima takribani 6 katika vijiji vitano vilivyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ambavyo vitagharimu kiasi cha Shilingi milioni 42.
* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad atembelea maghala ya kuhifadhia Karafuu kisiwani Pemba
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akiangalia karafuu zilizochakachuliwa kwa pamoja na unga wa makonyo, mchanga pamoja na maji katika Ghala la kuhifadhia karafuu Mkoani kisiwani Pemba,Kulia kwake ni Meneja Mkuu wa ZSTC HAMAD KHAMIS HAMAD na kushoto ni Mkuu wa Kusini Pemba JUMA KASSIM TINDWA.
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein afuturisha Wananchi wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Mtoto MUSSA MAKAME BADRU wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kufutari pamoja na wazee hao katika futari maalum aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akiwa katika futari na wananchi na wazee wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.
* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal azindua Ujenzi wa Maghorofa 30 ya Kambi ya Jeshi la Polisi Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akikata utepe kuzindua Maghorofa 30 ya Kambi ya Polisi yaliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, SHAMSI VUAI NAHODHA (kulia) ni Inspekta Jenerali wa Polisi, SAID MWEMA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Maghorofa 30 ya Kambi ya Polisi, Dakta HUBA NGULUMA.
Tuesday, August 9, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Mohammed Shein kwa nyakati tofauti amekutana na Balozi wa Nigeria nchini pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Mabohora Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dakta ISHAYA SAMAILA MAJANBU alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Balozi wa Nigeria Dakta ISHAYA SAMAILA MAJANBU kabla ya kuanza mazungumzo yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana Viongozi wa jumuiya ya Mabohora Zanzibar, wakiongozwa na Mwenyekiti AAMIL SAHEB SHEIKH SHABBIR ISMAIL walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana nae.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Mabohora Zanzibar, walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Monday, August 8, 2011
* Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi atembelea Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa
Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa Mkurugenzi wa Utafiti Dakta E. MPETA, pembeni ni afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo MONICA MUTONI,akifuatilia kwa karibu, katika banda la Mamlaka hiyo ndani ya Viwanja vya Nanenane mkoani Dodoma.
Subscribe to:
Posts (Atom)







