Sunday, July 31, 2011

* Mkutano wa Kamati kuu (CC) wa Chama cha Mapinduzi wafunguliwa Mjini Dodoma hii leo..


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA KIKWETE, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu, Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, WILLSON MUKAMA.


Mwenyekiti wa CCM taifa JAKAYA KIKWETE, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, AMAN ABEID KARUME (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, ALI HASSAN MWINYI (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, PIUS MSEKWA (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, WILLSON MUKAMA wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma mapema hii leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu Katikati ni Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA.

Wednesday, July 27, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal Auaga Mwili wa Marehemu Profesa Samuel Mushi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, SAMUEL MUSHI, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam,Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa SAMUEL MUSHI, wakati alipofika kuaga mwili wa Marehemu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa SAMUEL MUSHI.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, BENJAMIN WILLIAM MKAPA nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa SAMUEL MUSHI aliyefariki Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. 

Monday, July 25, 2011

* Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu azindua Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa


Waziri wa Uchukuzi OMARY NUNDU (kushoto) akiwa na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Uchukuzi OMARY NUNDU akiwa katika Picha ya Pamoja na Bodi Mpya ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.

* Rais Jakaya Kikwete Pamoja Viongozi Wengine wa Kitaifa Wahudhuria Sikukuu ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopigana Vita Nchini Msumbiji.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika ardhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiweka Ngao katika Mnara wa Mashujaa 1O1 walipozikwa ambao waliopigana vita  vya Msumbiji, ikiwa ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL Rais wa Zanzibar Dakta ALI MOHAMMED SHEIN wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigana Vita ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya mashujaa yaliyofanyika hii leo Mkoani Mtwara.


Rais JAKAYA KIKWETE na Makamu wake Dakta  MOHAMMED GHARIB BILAL wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja vya Naliendele Mkoani Mtwara.


Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe ya Kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania Waliopigana Vita Nchini Msumbiji.


Friday, July 22, 2011

* Maalim Seif akutana na Wachimbaji wa Matofali Kisiwani Pemba


Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akizungumza na wananchi na wachimbaji wa matofali huko Vitongoji Uwandani.


Naibu Katibu Mkuuu katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dakta ISLAM SEIF akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim SEIF juu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kufukia mashimo yaliyotokana na kazi za uchimbaji na upasuaji wa matofali Vitongoji Uwandani.


Kiongozi wa wachimbaji na wapasuaji wa matofali KOMBO ALI "Mbunge" akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, juu ya utekelezaji wa mpango wa kufukia mashimo yaliyotokana na kazi za uchimbaji wa matofali huko Vitongoji Uwandani.

Wednesday, July 20, 2011

* Rais Jakaya Kikwete aanza Ziara ya Kihistoria nchini Afrika Kusini

Rais JAKAYA KIKWETE akiwa pamoja na Rais wa Afrika Kusini Bwana JACOB ZUMA
Rais JAKAYA KIKWETE amesema mataifa ya Afrika bado yanahitaji misaada ya Ki-maendeleo, ingawa wajibu wa kujiendeleza unabakia mikononi mwao na sio kwa mataifa ya Kigeni wakiwamo wafadhili.

Rais KIKWETE ambae yupo Afrika Kusini kwa ziara ya Kihistoria tangu taifa hilo lilipopata uhuru mwaka 1994, amewataka wafanyabiashara na wawekezaji nchini humo kuanzisha vitega uchumi na kuwekeza katika uchumi wa Tanzania kwa sababu ya vivutio vikubwa vilivyopo hapa nchini.

Amesema umefika wakati kwa Tanzania na Afrika Kusini kutumia uhusiano wa kihistoria ili kujenga mahusiano imara na ya karibu zaidi ya kiuchumi baina ya nchi hizo.

Monday, July 18, 2011

* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akutana na Wakulima wa Karafuu Kisiwani Pemba


Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko AHMED MAZURI akitoa ufafanuzi juu ya mipango ya Wizara yake katika kufanikisha uchumaji wa zao la karafuu msimu huu. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba YAHYA BUGI akitoa amelezo kwa Makamu wa kwana wa Rais Maalim SEIF SHARIFF HAMAD juu ya mikakati ya Mkoa wake katika kupambana usafrishaji wa zao la karafuu kwa njia ya magendo.