Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika ardhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiweka Ngao katika Mnara wa Mashujaa 1O1 walipozikwa ambao waliopigana vita vya Msumbiji, ikiwa ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL Rais wa Zanzibar Dakta ALI MOHAMMED SHEIN wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigana Vita ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya mashujaa yaliyofanyika hii leo Mkoani Mtwara.
Rais JAKAYA KIKWETE na Makamu wake Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja vya Naliendele Mkoani Mtwara.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe ya Kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania Waliopigana Vita Nchini Msumbiji.
No comments:
Post a Comment