Saturday, July 2, 2011

* Shirika la Kimataifa la OXFAM lazindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula

Shirika la kimataifa la kukabiliana na umasikini wa Chakula la OXFAM limezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula,ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuwatambua na kuwaenzi wanawake wazalishaji wa Chakula.

Shindano hilo litawahusisha akina mama ambao ni wafugaji na wakulima wadogo wa mazao ya Chakula kutoka katika mikoa na maeneo mbalimbali hapa nchini.

Shindano hilo limezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Mcheza tamthilia maarufu ya Sex and the City kutoka Holywood nchini Marekani KRISTIN DAVIS huku akishirikiana na Balozi wa Kampeni ya Grow wa OXFAM ambae pia ni Mcheza Filamu wa Hapa nchini STEVEN KANUMBA.

Kwa mujibu wa OXFAM Shindano hilo litakuwa la wazi ambapo wananchi watakuwa wakishiriki kwa kuwapigia akina mama 10 watakaopita katika hatua ya awali mara baada ya kukamilisha utaratibu wa kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano hilo.


Kutoka kulia ni Mcheza filamu wa Tanzania STEVEN KANUMBA kati kati ni Mcheza tamthilia maarufu kutoka Holywood Marekani KRISTIN DAVIS aliyekaa upande wa Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la OXFAM,Tanzania Bi MONICA GORDON.


STEVEN KANUMBA kushoto akiwa pamoja na KRISTIN DAVIS mara baada ya Uzinduzi wa Nembo ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.

Mcheza Filamu na Balozi wa Kampeni ya Grow inayoratibiwa na Shirika la OXFAM hapa nchini STEVEN KANUMBA akicheza Ngoma mara baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment