Saturday, March 17, 2012

* Ujumbe wa kujitathmini Ki-Utawala Bora APRM wakutana na Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akizungumza na ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo


Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akifurahia jambo na Kiongozi wa Jopo la Wataalam kutoka Afrika wa Ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) AKERE TABENG MUNA (kulia) na Mwenyekiti wa Ujumbe huo kutoka Tanzania, HASA MLAWA (kushoto) baada kumaliza mazungumzo na Jopo hilo.


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Wajumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) baada kumaliza mazungumzo na Ujumbe huo.

Thursday, March 1, 2012

* Kocha wa Masumbwi Super D awafua Vijana wa Kambi ya Ilala



Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, RAJAB MHAMILA Super D (kulia) katika picha mbili tofauti akiwafundisha mabondia wa Kambi ya Ilala Jijini Dar es Salaam SAID MTITU pamoja na EMANNUEL MALOLO jinsi ya kutupa makonde.

Friday, February 24, 2012

Washiriki wa Halaiki ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar wakutana na Rais Shein




Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF ALI IDDI wakati wa hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.



Watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa wamevalia sare, wakisubiri kuanza kwa shughuli hiyo ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN.

Thursday, February 23, 2012

* Tanzania yasaini mkataba wa kupeleka washtakiwa wa Uharamia wa Ki-Somali katika Jela Husika



Rais JAKAYA KIKWETE na Waziri wa masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa na Afrika na Mazingira wa Uingereza HENDRY BELLINGHAM wakishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu.

Tuesday, February 21, 2012

* Waziri wa Habari Dakta Emmanuel Nchimbi awapatanisha Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi


Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI na Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakipeana mikono ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili,huku wapatanishi wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt EMMANUEL NCHIMBI(kushoto) pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU (kulia) wakishuhudia.


Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao.


Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili.

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal aendelea na ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa


Makamu wa Rais wa Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ASHA BILAL wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi.


Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, GEORGE MBAULA (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chief wa Kabila hilo.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akitembelea shamba la ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa.



Makamu wa rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, EXAVERY KAYANZA PINDA, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi.

Sunday, February 19, 2012

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal akutana na mtafiti wa Masokwe hapa nchini


Makamu wa Rais  Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akipokea zawadi ya kitabu cha mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, JANE GOODALL aliyefika Ikulu ndogo ya Wlaya ya Mpanda mkoa wa Katavi kwa ajili ya mazungumzo.

JANE amekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti katika mapori ya Gombe na Mahale yaliyopo mkoa wa Kigoma na Katavi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ASHA BILAL wakizungumza na Mtafiti bingwa wa Masokwe Duniani JANE GOODALL.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akielekezwa na mtafiti bingwa Duniani wa Masokwe, JANE GOODALL kuhusu ishara anazozitumia kuwasiliana na Masokwe na jinsi ya kuzungumza nao, wakati alipofika Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.