Makamu wa Rais wa Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ASHA BILAL wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi.
Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, GEORGE MBAULA (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chief wa Kabila hilo.
Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akitembelea shamba la ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa.
Makamu wa rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, EXAVERY KAYANZA PINDA, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi.
No comments:
Post a Comment