Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt ALI MOHAMMED SHEIN wa pili kushoto akiwa katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume MUHAMMAD s.a.w zilizofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh SALEH OMAR KABBI wa kwanza kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh OMAR OTHMAN MAKUNGU na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh KHAMIS HAJI.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt ALI MOHAMMED SHEIN katikati pamoja na Viongozi wengine wa wakiwa wamesima kumswalia Mtume MUHAMMAD s.a.w, wakati wa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwake na kumsifu katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama PILI BALOZI SEIF, pamoja na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume MUHAMMAD s.a.w zilizofanyika katika viwanja vya maisara Suleiman.
Wanafunzi wa Madrasa ya Qadiria ya el - Iman ya Tomondo Mjini Unguja wakisoma Qaswida ya Rabbi Swali ya kufungua Maulid ya kumsifu na kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume MUHAMMAD s.a.w.
No comments:
Post a Comment