Rais JAKAYA KIKWETE akiongoza matembezi ya Hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya akina mama ya Baobab iliyo chini ya CCBRT jijini Dar es salaam.
Katika picha kutoka kulia Meya wa Ilala JERRY SLAA, Meya wa Kinondoni Bwana MWENDA, Bwana ERWIN TELEMANS Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, RENE MEZA Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bwana WILBROAD SLAA na kulia kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dakta HADJI MPONDA na Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Bwana ANDREW DUNNET pamoja na MWAMVITA MAKAMBA wa Vodacom Tanzania wakiwa katika matembezi hayo.
Rais JAKAYA KIKWETE akishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuongoza matembezi ya hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya akina mama wenye matatizo mbalimbali ya uzazi katika hospitali ya CCBRT.
Matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa Find your Moyo.
No comments:
Post a Comment