Rais JAKAYA KIKWETE na mkewe mama SALMA KIKWETE wakimjulia hali Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali ERNEST MWITA KYARO jijini Mwanza, Jenerali mstaafu KYARO, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi katika Serikali ya awamu ya kwanza, amefurahi na kumshukuru sana Rais KIKWETE na mkewe kwa kutembelea.
Rais JAKAYA KIKWETE akiongea na wawakilishi wa kundi moja la wachuuzi machinga wa jijini Mwanza ambao walikwenda Ikulu ndogo ya jiji hilo na kumweleza changamoto zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji pamoja na taaluma ya kufanyia biashara.
Rais KIKWETE ametoa milioni 10 kwa ajili yawamachinga hao kukopeshana mitaji.
No comments:
Post a Comment