Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI na Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakipeana mikono ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili,huku wapatanishi wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt EMMANUEL NCHIMBI(kushoto) pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU (kulia) wakishuhudia.
Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili.
No comments:
Post a Comment