Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj ALI HASSAN MWINYI wakiwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushirikisha jumla ya washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an JAHUDDIN ADAM kutoka Sudan mara baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj ALI HASSAN MWINYI pamoja na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.