Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Finland nchini Tanzania, SINIKKA ANTILA ,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Wednesday, October 26, 2011
* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal ahudhuria na kutembelea Banda la Tanzania wakati wa mkutano wa Kimataifa wa mawasiliano ITU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa ITU uliofanyika Geneva Switzelrand.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) PETER MASIKA kuhusu namna ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta, wakati akikagua banda la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) ambao umefanyika Geneva, Switzerland.
Monday, October 24, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein aapishwa na kuwa mjumbe wa kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akipokea hati ya kiapo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN baada ya kuapa kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, MOHAMMED CHANDE OTHMAN kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu namba 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wote.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALl MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE mara baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuesday, October 18, 2011
* Ajali ya moto yateketeza maduka manne Singida mjini
Picha mbili tofauti zikionesha tukio la moto pamoja na jitihada za kikosi cha zimamoto katika kukabiliana na moto huo ili usisambae kwenda katika maduka mengine.
Sunday, October 16, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein atembelea vikundi vya wajasiriamali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akiangalia maonesho ya bidhaa mbali mbali za vikundi vya ushirika vya akinamama,katika viwanja vya Salama Bwawani Hoteli,ikiwa ni njia moja ya kuvitangaza vikundi hivi katika mkutano wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliomalizika jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akipata maelezo kutoka kwa SAIDA ALI MOHAMMED wa Wizara ya Ustawi wa Jamii maendeleo ya wanawake na watoto wakati alipotembelea maonesho ya bidhaa mbali mbali za vikundi vya ushirika vya akinamama.
Rais wa Shirika la African Investiment Corporation ambae pia mtendaji mkuu kutoka Marekani Daniel Anagho akitoa mada inayohusu Masuala ya utalii katika mkutano wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliomalizika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Saturday, October 15, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein ahudhuria mkutano wa Jumuia ya Wafanya Biashara na wenye viwanda ZBC
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya wafanya Biashara wenye viwanda na wakulima ZBC MBAROUK OMAR wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na wadau mbali mbali katika mkutano wa siku mbili wa Baraza la Biashara ZBC(kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, NASSOR AHMED MAZRUI na (kulia) ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi ABDIHAMID YAHAYA MZEE.
Wadau mbalimbali walioalikwa katika mkutano wa Baraza la Biashara chini ya uenyekiti wake Dk ALI MOHAMMED SHEIN wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Salama Bwawani Hotel wakisikiliza mada mbalimbali zilizotolewa katika mkutano huo wa siku mbili.
Thursday, October 13, 2011
* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal azindua kituo cha kulelea watoto yatima
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akikata utepe kuzindua rasmi Kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Full Gospel Children’s Home, kilichopo Msongola Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wakitoa burudani ya kuigiza maisha ya watoto waishio katika mazingira magumu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Full Gospel Children’s Home.
Wednesday, October 12, 2011
* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein awapongeza wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 waliofanya vizuri visiwani Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na walimu na wanafunzi bora wa kidato cha nne na sita,waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2010-2011,alipokutana nao katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal atoa Pole kwa Familia ya Balozi Juma Mwapachu Jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha HARITH MWAPACHU, ambaye ni mtoto wa Balozi JUMA MWAPACHU, aliyefariki dunia Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)