Wednesday, June 13, 2012

* Mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba Kuzichapa Julai 7 mwaka huu


Mabondia FRANCIS CHEKA (kushoto) na JAPHET KASEBA wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Julai 7 katika uwanja mpya wa taifa ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Diamond.

Pia kutakua na mechi ya Bongo Movie na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na KAIKE SIRAJU utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpambano huo ni  Adiphoce Mchumia tumbo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali huku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na  Said Mbelwa wakati bondia chipukizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D'  watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba.

Friday, June 8, 2012

* Rais Jakaya Kikwete awaapisha Majaji wawili na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama



Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akimwapisha SEMISTOCLES KAIJAGE (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Kabla ya uteuzi huo KAIJAGE alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.

Jaji wa Mahakama ya Rufani MUSSA KIPENKA akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais  Dkt JAKAYA KIKWETE Ikulu jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania MOHAMMED CHANDE OTHMAN.

Rais JAKAYA KIKWETE akimwapisha EDWARD RUTAKANGWA kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dares Salaam.

* Rais Dakta Ali Shein kwa Nyakati tofauti akutana na Balozi wa Sweden, pia ameagana na Balozi wa Msumbiji aliyemaliza muda wake


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania AMOUR ZAKARIA aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania LENNARTH HJELMAKER aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa  Rais.

Thursday, June 7, 2012

* Kampuni ya Simu ya tiGO yatoa Zawadi na Burudani Mbalimbali kwa Wateja wake Wilayani Babati





Picha hizi zinaonyesha matukio mbalimbali yaliyofanyika wilayani Babati, ambapo kampuni ya tiGo iliwapatia wateja burudani kutoka kwa mwanamuziki H.Baba , Pia wateja walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali kutoka kwenye vibanda vya tiGo vilivyopatikana viwanjani hapo, ambapo Zawadi kama T-shirt za tiGo, Simu na kofia zilitolewa katika tamasha hilo.

* Rais Kikwete pamoja na makamu wake Dakta Bilal,kwa nyakati tofauti wameagana na Balozi wa Canada aliyemaliza muda wake



Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Bwana ROBERT J. ORR ambae amemaliza muda wake wa uwakilishi, katika Ikulu ya Mjini Dar es Salaam.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILALakizungumza na Balozi wa Canada ROBERT J. ORR, aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

* Vijana wa CCM Temeke, wachukua fomu za Kugombea Uenyekiti Wilayani humo


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (CCM) UVCCM wilaya ya Temeke PIUS SELEMAN 'Pukapuka' akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Uwenyekiti wa Umoja huo Wilayani humo, Bwana ATHUMANI NYAMLAN Dar es Salaam, anaeshudia katikati ni Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Sandali Bwana RAMADHANI MGOMI.

* Kampuni ya Simu ya Tigo yazindua Huduma ya "tiGO Internet Mega Boksi"


Tigo Public Relations Officer, ALICE MARO (right) and KWAME MAKUNDI Manager, Operations Internet Services, listening to questions from the media during the Tigo Internet Mega Boksi press conference.


KWAME MAKUNDI (left), Manager Operations Internet Services, explaining the new Tigo Internet services to the media, while ALICE MARO, Tigo Public Relations Officer listens in.