Mabondia FRANCIS CHEKA (kushoto) na JAPHET KASEBA wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Julai 7 katika uwanja mpya wa taifa ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Diamond.
Pia kutakua na mechi ya Bongo Movie na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na KAIKE SIRAJU utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpambano huo ni Adiphoce Mchumia tumbo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali huku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipukizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba.

No comments:
Post a Comment