Saturday, December 31, 2011

* Rais Jakaya Kikwete amuapisha Balozi Ombeni Yohana kuwa katibu mkuu kiongozi Mpya



Rais JAKAYA KIKWETE, akimuapisha rasmi Balozi OMBENI YOHANA SEFUE kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, aliyemaliza muda wake.


Rais JAKAYA KIKWETE, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL,Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA na Balozi Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, PHILLEMON LUHANJO, mara baada ya kuapishwa na Rais KIKWETE kuwa katibu mkuu kiongozi mpya.


Rais JAKAYA KIKWETE, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi OMBENI YOHANA, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein atoa Salamu za Mwaka mpya kwa Watanzania



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akitoa salamu za kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 Biladiya, kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kuwatakia amani na utulivu, ambapo amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali yao kwa michango mbali mbali katika jitihada za kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.

Friday, December 30, 2011

* Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC John Ngahyoma afariki Dunia Jijini Dar es Salaam

Marehemu JOHN NGAHYOMA enzi ya Uhai wake

Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ya Uingereza, JOHN NGAHYOMA amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake eneo la Segerea Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Familia ya NGAHYOMA imesema kwamba Marehemu JOHN alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kansa katika ini iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu, ambapo amewahi kwenda kutibiwa mara mbili nchini INDIA.

Marehemu NGAHYOMA anatazamiwa kuzikwa siku ya Jumapili katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

* Rais Jakaya Kikwete atoa Heshima za Mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji wa TBC, Halima Mchuka


Rais JAKAYA KIKWETE na waombolezaji wakiombea mwili wa HALIMA MCHUKA
Aliyekuwa mtangazaji wa TBC Hayati Bi HALIMA MCHUKA


Rais JAKAYA KIKWETE akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji HALIMA MCHUKA leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa.

Rais JAKAYA KIKWETE akiwapa pole wafiwa

Wednesday, December 28, 2011

* Dakta Ali Shein ahudhuria mazishi ya kanal Nassor Waziri Mageta


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt ALI MOHAMMED SHEIN (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiusalia mwili wa Marehemu Kanal NASSOR WAZIRI MAGETA aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia katika msikiti wa masjid Twariq Bububu nje wa mji wa Zanzibar, aliyefariki jana na kuzikwa Kijijini kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Askari wa Vikosi vya SMZ wakilibeba Jeneza lenye mwili waMarehemu Kanal NASSOR WAZIRI MAGETA aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Alhaj Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akitia udongo katika kaburi la Marehemu Kanal NASSOR WAZIRI MAGETA.


Askari wa Vikosi vya SMZ wakitoa salamu ya hesha katika kaburi la marehemu Kanali NASSOR WAZIRI MAGETA aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia.

Tuesday, December 27, 2011

* Mamlaka ya hali ya Hewa yatoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa mvua kali kuanzia Disemba 27 mpaka Januari 2012




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa na mvua kuanzia mwezi Desemba 27, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012. Ukanda wa mvua unatarajiwa kuimarika maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani kesho ukiwemo mkoa wa Dar es salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya 2012.

Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi,sambamba na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na kusababisha makutano ya upepo katika eneo la mashariki na kusini magharibi mwa nchi kuanzia Disemba 28, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012.

Hali hii inatarajiwa kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.


Picha tofauti za mawingu na Bahari zilizopigwa kupitia Satelite zikionesha hali ya uwezekano wa kuwepo kwa Mvua kali zinazotarajiwa kunyesha hapa nchini.

Maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwani( mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Kisiwa cha Unguja,), Nyanda za juu kusini magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa), kanda ya kati(Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) na maeneo machache ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki (mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua kubwa.

Kufuatia viwango vikubwa vya mvua vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu. Mamlaka inashauri tahadhari stahiki ziendelee kuzingatiwa.

Maeneo mengine ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za kawaida katika kipindi hicho.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa na tahadhari kila inapobidi.

Saturday, December 24, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal awatembelea waathirika wa mafuriko ya Mvua Jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam MECKY SADICK (kulia) wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo eneo la Jangwani.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na Bi MONICA LUIS Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi. 

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein ahudhuria Mahafali ya 7 SUZA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambae pia ni mkuu wa Chuo kikuu cha taifa SUZA Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akimtunuku shahada ya uzamivu ya heshima ya chuo hicho, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dakta AMANI ABEID KARUME wakati wa sherehe za mahafali ya 7 ya chuo hicho katika viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Friday, December 23, 2011

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein afungua Masjid Rashidin


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk ALI MOHAMMED SHEIN akiufungua Masjid Rashidin wa Dole Wilaya ya Magharibi mara baada ya kuwasili katika maeneo ya msikiti huo Uliopo Kijijini hapo.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Dole Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kuufungua msikiti wa Masjid Rashidin.

* Walk for water yakabidhi Visima 6 Bagamoyo



Mwisho wa mwaka 2011 utaleta furaha mpya na matumaini kwa vijiji 6 kufuatia makabidhiano ya visima 6 katika maeneo mbalimbali yenye uhaba wa maji katika kanda ya Bagamoyo kupitia mradi wa Walk for Water-mpango wa Spearhead Africa Limited. Visima 6 ni msaada kutoka Belgian Technical Co-operation, Tanzania Distillers Limited na mradi wa Walk for Water.

Baada ya miezi 8 mfululizo ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kukamilisha lengo la mradi wa Walk for Water 2011, sasa mradi huu umefikia hatua za mwisho katika ujenzi wa visima 6 katika maeneo tofauti yenye uhaba wa maji katika ukanda wa Bagamoyo. Lengo la mpango kwa mwaka 2011 ni kujenga uelewa wa uhaba wa maji kimataifa na ndani ya nchi na kujenga visima na kupata vituo vya upatikanaji maji katika vijiji vya Bagamoyo kwa msaada wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.

Mpango huu unaonyesha nguvu ya ushirikiano wa sekta ya umma binafsi katika kubadili maisha ya baadhi ya watanzania wenye matatizo mbalimbali na kwa juhudi ya pamoja kutoa baadhi ya huduma za msingi kwa jamii. Kwa lengo la kuleta mabadiliko kwa watu wenye bahati ya chini, visima hivi vitasaidia wakazi wa Bagamoyo katika kupata maji safi na salama si tu kwa ajili ya shughuli zao za kila siku lakini pia katika kudumisha afya na masuala ya usafi wa mazingira katika vijiji.

Kufanya kazi kwa kushirikiana na ofisi ya Manispaa ya Bagamoyo, Ifakara Health Institute-waanzilishi wenza wa mradi wa Walk For Water 2011, imeanzisha Kamati za Maji katika kila kijiji kwenye vijiji vyote 6. Kamati imeundwa kwa ajili ya matengenezo endelevu ya kisima. Wanachama wa Kamati ya Maji watapewa kitabu na mafunzo yanayohitajika kutoka kwa wenza wetu Ifakara Health Institute juu ya kudumisha kisima na itakuwa na wajibu wa kuhakikisha matumizi sahihi ya maji ya wanakijiji.

Wakati wa uzinduzi wa moja ya visima, bi. Bertha Ikua-Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Spearhead Africa Limited alisema “Tungependa kutoa shukrani zetu kwa Tanzania Distillers Limited na Belgian Development Co-operation na wote walioshiriki katika tukio la Walk for Water na kudhamini visima vilivyojengwa chini ya mradi wa Walk for water. Tungependa pia kuwashukuru Dr Salim Abdulla-Mkurugenzi wa Ifakara Health Institute na Mr. Peter Sasse kwa kushirikiana nasi katika juhudi hii-muda wao wa thamani na kujitolea kwao sio tu unashukuriwa na sisi, bali pia na wanawake na watoto wa kijiji hiki”.

“Shukrani zetu zimuendee Bi Margaret Masanga-katibu wa mbunge Ofisi ya Manispaa ya Bagamoyo kwa muda wake na kujitolea kwa kutoa msaada katika kutambua maeneo muhimu ambayo yana haja ya maji, pia, kwa kusaidia upatikanaji wa vibali na nyaraka na kurasimisha kisima pamoja na manispaa na kamati na kwa msaada wao mkubwa katika mradi huo.”

Uchimbaji wa visima hivi 6 ni ushahidi tosha wa kauli mbiu ya mradi wa Walk for Water:Kila hatua ina thamani. Kila tone lina thamani.Kila mchango una thamani. Mpango huu unahamasisha wabia wengine kujiunga na miradi kama hii ili kuleta tofauti katika maeneo yenye mahitaji.

Tuesday, December 13, 2011

* Dakta Jakaya Kikwete atembelea maonesho ya miaka 50 ya Uhuru ndani ya Viwanja vya Saba saba


Rais JAKAYA KIKWETE akisaini kitabu cha wageni katika banda la Benki Kuu ya Tanzania BOT.


Rais JAKAYA KIKWETE akiwa ndani ya Banda la Mamlaka ya mapato Tanzania TRA.


Rais JAKAYA KIKWETE akipata maelezo ya mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali kwenye  banda la Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ.


Rais JAKAYA KIKWETE akiongea na wanafunzi wa Sekondari ya VERSITY kuhusu maabara ya Sayansi.
.

Rais JAKAYA KIKWETE akitembelea bustani ya wanyama pori katika banda la Wizara ya Maliasili na utalii.

Wednesday, November 30, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal afunga mkutano wa nchi za maziwa makuu mjini Bujumbura


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt JAMES MWASI baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu.


Waziri wa Afrika Mashariki, SAMUEL SITTA akiwa katika Ukumbi wa Golf akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL alipokuwa akifunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliomalizika mjini Bujumbura nchini Burundi.

Monday, November 28, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal afungua Mkutano wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga CHIKU GALAWA na waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, MATHIAS CHIKAWE.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA mara baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa Viongozi wa Takukuru.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED BILAL akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, EDWARD HOSEA wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru, uliofanyika Mkoani Tanga Kushoto ni waziri wa Ofisi ya Rais- Utawala Bora, MATHIAS CHIKAWE.


Baadhi ya Wakuu wa Vitengo wa Takukuru waliohudhuria Mkutano huo Mkuu wa Mwaka ulioanza leo Novemba 28 na kumalizika kesho, Mkoani Tanga.

Saturday, November 26, 2011

* Mwakilishi wa UNDP amaliza muda wake wa kazi hapa nchini


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na mwakilishi wa Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP anayeishi Visiwani humo, SORO KARNA aliyefika Ikulu ya Mjini Zanzibar kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi hapa nchini.

Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na mwakilishi wa UNDP Bwana SORO KARNA aliyefika Ikulu ya Mjini Zanzibar kumuaga Rais.

* Makamu wa Rais Dakta Gharib Bilal azindua Tamasha la utamaduni wa Mtanzania


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa baada ya uzinduzi wa tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania ndani ya kijiji cha Makumbusho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimsikiliza Waziri Mkuu MIZENGO PINDA wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akimshuhudia Waziri Mkuu MIZENGO PINDA akinywa kinywaji cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

* Mahafali ya Pili ya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM yafana


Kiongozi wa timu ya Viongozi wa Juu wa UDOM wakiwa katika Maandamano ya kuelekea kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.


Baadhi ya Viongozi chuo kikuu cha Dodoma wakiwa tayari kwenye Maandamano kuelekea kwenye Mahafali ya Pili ya chuo hicho.


Viongozi wa chuo kikuu cha Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa chuo hicho Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BENJAMIN WILLIAM MKAPA wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa unaimbwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM


Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sosholojia wakiwa katika furaha Mara baada ya kutunukiwa Shahada zao.