Sunday, July 31, 2011

* Mkutano wa Kamati kuu (CC) wa Chama cha Mapinduzi wafunguliwa Mjini Dodoma hii leo..


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA KIKWETE, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu, Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, WILLSON MUKAMA.


Mwenyekiti wa CCM taifa JAKAYA KIKWETE, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, AMAN ABEID KARUME (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, ALI HASSAN MWINYI (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, PIUS MSEKWA (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, WILLSON MUKAMA wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma mapema hii leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu Katikati ni Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA.

Wednesday, July 27, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal Auaga Mwili wa Marehemu Profesa Samuel Mushi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, SAMUEL MUSHI, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam,Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa SAMUEL MUSHI, wakati alipofika kuaga mwili wa Marehemu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa SAMUEL MUSHI.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, BENJAMIN WILLIAM MKAPA nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa SAMUEL MUSHI aliyefariki Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. 

Monday, July 25, 2011

* Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu azindua Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa


Waziri wa Uchukuzi OMARY NUNDU (kushoto) akiwa na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Uchukuzi OMARY NUNDU akiwa katika Picha ya Pamoja na Bodi Mpya ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.

* Rais Jakaya Kikwete Pamoja Viongozi Wengine wa Kitaifa Wahudhuria Sikukuu ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopigana Vita Nchini Msumbiji.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika ardhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE akiweka Ngao katika Mnara wa Mashujaa 1O1 walipozikwa ambao waliopigana vita  vya Msumbiji, ikiwa ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL Rais wa Zanzibar Dakta ALI MOHAMMED SHEIN wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigana Vita ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya mashujaa yaliyofanyika hii leo Mkoani Mtwara.


Rais JAKAYA KIKWETE na Makamu wake Dakta  MOHAMMED GHARIB BILAL wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja vya Naliendele Mkoani Mtwara.


Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe ya Kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania Waliopigana Vita Nchini Msumbiji.


Friday, July 22, 2011

* Maalim Seif akutana na Wachimbaji wa Matofali Kisiwani Pemba


Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akizungumza na wananchi na wachimbaji wa matofali huko Vitongoji Uwandani.


Naibu Katibu Mkuuu katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dakta ISLAM SEIF akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim SEIF juu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kufukia mashimo yaliyotokana na kazi za uchimbaji na upasuaji wa matofali Vitongoji Uwandani.


Kiongozi wa wachimbaji na wapasuaji wa matofali KOMBO ALI "Mbunge" akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, juu ya utekelezaji wa mpango wa kufukia mashimo yaliyotokana na kazi za uchimbaji wa matofali huko Vitongoji Uwandani.

Wednesday, July 20, 2011

* Rais Jakaya Kikwete aanza Ziara ya Kihistoria nchini Afrika Kusini

Rais JAKAYA KIKWETE akiwa pamoja na Rais wa Afrika Kusini Bwana JACOB ZUMA
Rais JAKAYA KIKWETE amesema mataifa ya Afrika bado yanahitaji misaada ya Ki-maendeleo, ingawa wajibu wa kujiendeleza unabakia mikononi mwao na sio kwa mataifa ya Kigeni wakiwamo wafadhili.

Rais KIKWETE ambae yupo Afrika Kusini kwa ziara ya Kihistoria tangu taifa hilo lilipopata uhuru mwaka 1994, amewataka wafanyabiashara na wawekezaji nchini humo kuanzisha vitega uchumi na kuwekeza katika uchumi wa Tanzania kwa sababu ya vivutio vikubwa vilivyopo hapa nchini.

Amesema umefika wakati kwa Tanzania na Afrika Kusini kutumia uhusiano wa kihistoria ili kujenga mahusiano imara na ya karibu zaidi ya kiuchumi baina ya nchi hizo.

Monday, July 18, 2011

* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akutana na Wakulima wa Karafuu Kisiwani Pemba


Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko AHMED MAZURI akitoa ufafanuzi juu ya mipango ya Wizara yake katika kufanikisha uchumaji wa zao la karafuu msimu huu. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba YAHYA BUGI akitoa amelezo kwa Makamu wa kwana wa Rais Maalim SEIF SHARIFF HAMAD juu ya mikakati ya Mkoa wake katika kupambana usafrishaji wa zao la karafuu kwa njia ya magendo.

Friday, July 15, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal na Rais wa Mfuko wa Kuwait Kanda ya AFRIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Rais wa Mfuko wa Kuwait Ukanda wa Afrika Sheikh FAHDI MOHAMMED AL-SHAMRI wakati alipofika kumtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akizungumza na Rais wa Mfuko wa Kuwait Ukanda wa Afrika, Sheikh FAHDI MOHAMMED AL-SHAMRI wakati alipofika kumtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa upande wa Tanzania SAMY MOHAMMED.




Wednesday, July 13, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal afungua Mkutano mkuu wa tatu wa Baraza la wakuu wa Vyuo vikuu huria AFRIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa tatu wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya Masafa unaohudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.


Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakifuatilia hotuba ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika.

Tuesday, July 12, 2011

* Maalim Seif Shariff Hamad Akutana na Mfalme wa Ashanti Visiwani Zanzibar

Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akizungumza na Mfalme wa Ashanti, OTUMFUO OSEI TUTU ofisini kwake Migombani, Zanzibar

Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akipokea zawadi kutoka kwa msaidizi wa Mfalme wa Ashanti, OTUMFUO OSEI TUTU, baada ya kumaliza mazungumzo yao,ofisini kwake Migombani Zanzibar


Monday, July 11, 2011

* Maalim Seif Shariff Hamad afungua Jengo la uendeshaji Mashtaka


Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Uendeshaji Mashtaka kitengo cha Uendeshaji mashtaka Mahakama za Wilaya huko Mwanakwereke Wilaya ya Magharibi Unguja.

* Maalim Seif Shariff Hamad Akutana na wananchi wa Kijiji cha Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja


Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada kumaliza ziara yake ya Kichama kuzungumza na Viongozi wa Jimbo la Ngungwi.


Friday, July 8, 2011

* Simba na Yanga Zatinga Fainali ya Michuano ya Kombe la Kagame,Kukipiga Jumapili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

  
 
Rais wa Rwanda PAUL KAGAME ndie Mdhamini wa Michuano ya Kombe la Kagame


Kikosi cha Timu ya SIMBA Sports Club  ambao ni maarufu kama Wekundu wa Msimbazi watakaokipiga na Mahasimu wao wakubwa YANGA Sports Club watoto wa Jangwani katika Fainali ya Kombe la Kagame.


Kikosi kamili YANGA Sports Club ambao ni maarufu kwa jina la watoto wa Wajangwani ambao watakabiliana na mahasimu wao wa Enzi SIMBA Sports Club katika Michuano ya Kombe la Kagame itakayopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, July 6, 2011

* Mtoto Felix Finkbeiner akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Tayari kuanza Ziara yake ya kupanda miti katika Shule za Msingi hapa nchini


Mtoto FELIX FINKBEINER kutoka Nchini Ujerumani  Kulia akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akiwa tayari kuanza Ziara ya Upandaji wa Miti katika Shule za Msingi kupitia kampeni yake inayoitwa Plant the Planet Stop talking ambapo anatazamiwa kuelekea Visiwani Zanzibar na Baadae ataenda mkoani Arusha pia anatazamiwa kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa katika ziara yake hapa nchini.

Tuesday, July 5, 2011

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZANZIBAR Maalim Seif Shariff Hamad Wakutana katika Viwanja vya Saba saba.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

* Mashindano ya Pikipiki yafana Viwanja vya Tanganyika Packers kawe Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii


Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.


Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Waendesha Pikipiki, Adil Othman (mbele) akichuana na Ludan Volvo, wakati wa mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Adil ni mtaalam wa kutumia Pikipiki yenye matairi manne aina ya Quad Bike na Volvo ni mtaalam katika pikipiki ya matairi mawili, hapa wakionyeshana ujuzi.

                                    


Saturday, July 2, 2011

* Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL azindua rasmi Maonesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL, akizindua rasmi maonyesho ya 35 ya Biashara  ya Kimataifa , wakati alipotembeleea maonyesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL akimkabidhi Tuzo ya ushindi wa kundi la Engineering Products Mkurugenzi Mkuu wa Sido, MIKE LAISER,wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Mjomba MRISHO MPOTO akitoa burudani mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.

* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akutana na Wakurugenzi wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar

 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim SEIF SHARIF HAMAD akipokea Kabrasha la mpango mkakati la maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, ISSA AHMEID OTHMAN ofisini kwake Migombani.

* Shirika la Kimataifa la OXFAM lazindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula

Shirika la kimataifa la kukabiliana na umasikini wa Chakula la OXFAM limezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula,ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuwatambua na kuwaenzi wanawake wazalishaji wa Chakula.

Shindano hilo litawahusisha akina mama ambao ni wafugaji na wakulima wadogo wa mazao ya Chakula kutoka katika mikoa na maeneo mbalimbali hapa nchini.

Shindano hilo limezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Mcheza tamthilia maarufu ya Sex and the City kutoka Holywood nchini Marekani KRISTIN DAVIS huku akishirikiana na Balozi wa Kampeni ya Grow wa OXFAM ambae pia ni Mcheza Filamu wa Hapa nchini STEVEN KANUMBA.

Kwa mujibu wa OXFAM Shindano hilo litakuwa la wazi ambapo wananchi watakuwa wakishiriki kwa kuwapigia akina mama 10 watakaopita katika hatua ya awali mara baada ya kukamilisha utaratibu wa kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano hilo.


Kutoka kulia ni Mcheza filamu wa Tanzania STEVEN KANUMBA kati kati ni Mcheza tamthilia maarufu kutoka Holywood Marekani KRISTIN DAVIS aliyekaa upande wa Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la OXFAM,Tanzania Bi MONICA GORDON.


STEVEN KANUMBA kushoto akiwa pamoja na KRISTIN DAVIS mara baada ya Uzinduzi wa Nembo ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.

Mcheza Filamu na Balozi wa Kampeni ya Grow inayoratibiwa na Shirika la OXFAM hapa nchini STEVEN KANUMBA akicheza Ngoma mara baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Jijini Dar es Salaam.