Wednesday, June 29, 2011

* Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL amekutana na Balozi wa VIETNAM NGUYEN DUY THIEN katika Ikulu ya Mjini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Duy Thien, wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tuesday, June 28, 2011

* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akutana na Balozi wa Marekani hapa nchini ALFONSO LENHARDT


Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt ofisini kwake Migombani ambapo pamoja na mambo mengine aliiomba Marekani kuunga mkono juhudi za Serikali ya Zanzibar katika vita dhidi ya uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.

* Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL kwa Nyakati tofauti akutana na Mabalozi kutoka Nchi za Kenya, Sudan pamoja na Zambia katika Ikulu ya Mjini Dar es Salaam



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania, Abdelbagi Hamdan Kabeir wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam na kufanya mazungumzo.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, John Mutinda Mutiso, wakati alipofika kumtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam  Kushoto ni Msaidizi wa Balozi, Muthomi Muithiga.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mavis Lengalenga, baada ya mazungumzo wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam.

Monday, June 27, 2011

* Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akutana na Wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika Chuo kikuu cha Waislamu cha Morogoro

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim SEIF SHARIFF HAMAD akizungumza na wahitimu watarajiwa wa Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha Waislamu, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kanal Mstaafu ISSA MACHIBYA


Sunday, June 26, 2011

* Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB BILAL awa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ta Kitaifa ya kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo.

Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Rashid Abdallah wa IOGT  wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya.


Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam Juni 26, 2011.

Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.