Thursday, April 26, 2012

* Mabondia Japhet Kaseba na Francis Cheka kupambana siku ya Saba saba

Bingwa Mchezo wa Kickboxing hapa nchini JAPHET KASEBA akisaini mkataba wa kupambana na FRANCIS CHEKA.


Bondia FRANCIS CHEKA akisaini mkataba wa kupambana na JAPHET KASEBA.


Na Mwandishi wetu

Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukuru kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanataka kupigana nae.



Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae.
"Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu" alisema Cheka.

"Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kiporo".

Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao haujawahi kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi
.

* Kichanga chaokotwa kitongoji cha Isevya Mkoani Tabora

Kichanga kikiwa kimetupwa na mtu ambae mpaka sasa bado hajafahamika eneo la Isevya mkoani Tabora.


Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora wakijadiliana Jambo kuhusu Tukio hilo. 

Dampo ambalo kitoto hicho kichanga kilitupwa , pembeni ni Baadhi ya wananchi pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi wakipata maelezo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.



Umati wa Wananchi wa eneo la Isevya Mkoani Tabora wakishuhudia tukio hilo la kutupwa kwa Kichanga.


Na Mwandishi wetu

Mtu asiyejulikana amekitupa kitoto kichanga kwenye dampo lililopo kwenye Soko la kata ya Isevya manispaa ya Tabora

Kichanga hicho  kinachokadiriwa kuwa na umri kati ya miezi nane na tisa kimeokotwa na mtu anayedaiwa kuwa na magonjwa ya akili ambaye alikwenda kutupa takataka katika dampo hilo na kukikuta kichanga hicho kikiwa kimefunikwa na khanga.

Hata hivyo mtu huyo anayefahamika soko la Isevya kwa kazi ya kubeba takataka,baada ya kugundua kichanga hicho kilichotapakaa damu nyingi alikichukua na kukipeleka sokoni hapo huku akilalamikia kitendo cha kutupwa kichanga hicho ambacho hakikuwa na uhai.

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Isevya walistaajabu tukio hilo huku zikiwashangaza zaidi kauli za mtu huyo ambaye huwa wakimfahamu kwa mapungufu ya akili.

Kwa upande mwingine maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho huku wakiwaomba wananchi kutoa taarifa za mtu atakayebainika kuwa amehusika na tukio hilo la kinyama.
 
Hata hivyo katika kata ya Isevya matukio utoaji mimba na kutupa watoto yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ingawa mara nyingi wanaojihusisha na matendo hayo wamekuwa wakifichwa.

Wednesday, April 25, 2012

* Bondia Cheka ajifua kumchakaza Maugo Jumamosi hii


Kocha wa ngumi ABDALLAH ILAMBA 'Komando' akimsimamia Bondia FRANCIS CHEKA kufanya mazoezi ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake na MADA MAUGO wa kugombea mkanda wa I.B.F pamoja na gari utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba.

Saturday, April 21, 2012

* Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wameuwawa Jijini Dar es Salaam

DCP - SULEYMAN KOVA
Na Mwandishi
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokutwa wakiwa na silaha tatu, ambao walikuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katikati ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo DCP-SULEYMAN KOVA amesema watu hao wameuawa katika majibizano ya Risasi na Kikosi maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na Ujambazi.
Amesema kuuliwa kwa watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi kumetokana na Jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa wananchi kupitia mpango wa Polisi Jamii.
Kamanda KOVA amesema baada ya Jeshi hilo kupokea taarifa hizo walizifuatilia na kuwakuta watu hao wakiwa katika baa iliyotajwa kwa Jina la Respect mabibo wakijiandaa kwa minajili ya kwenda kutekeleaza uhalifu.
Amesema katika tukio hilo hakuna Askari wala Raia alijeruhiwa katika tukio hilo ambalo limetokea jana majira ya mchana eneo la Mburahati Madoto.

Friday, April 20, 2012

* Rais Jakaya Kikwete amaliza Ziara ya kikazi nchini Brazil


Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa chama cha wafanya biashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo.


Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika mazungumzo na viongozi wa chama cha wafanya biashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo.
 
Wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa chama hicho Bwana JOAO GUILHERME na kushoto ni Mkurugenzi wa chama hicho THOMAZ ZANOTTO na kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mheshimiwa HAROUN ALI SULEIMAN.

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein azindua tanki la Maji safi wilaya ya Chake Chake Pemba



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba.



Baadhi ya wananchi wa shehia ya ziwani na vijiji jirani wakimsikiliza,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt ALI MOHAMMED SHEIN,alipokua akizungumza nao wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba.

* Viongozi wa madhehebu ya Dini wapigwa msasa kuhusu Sensa ya watu na makazi ya 2012


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi RAMADHAN KHIJJAH akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.



Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi RAMADHAN KHIJJAH alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi RAMADHAN KHIJJAH (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012

Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. ALBINA CHUWA (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat AMINA MRISHO.

Thursday, April 19, 2012

* Mambo safi Group yaweka kambi kwa ajili ya makamuzi ya MAY DAY


Mkurugenzi wa SF GROOUP OF COMPANIES LIMITED, SELINA KOKA kushoto akimkabidhi gita kiongozi wa kundi la Mambo safi, FABBIAN SALVATORY 'Super Phabby' kwa ajili ya kuweka kambi ya siku saba ili waanze kutoa burudan kwa wakazi wa jiji ifikapo mei mosi mwaka huu.


Mkurugenzi wa SF GROOUP OF COMPANIES LIMITED, SELINA KOKA kushoto akiwa pamoja na kundi la Mambo Safi.

Na Mwandishi Wetu
KUNDI la muziki wa asili na dansi la Mambo Safi  limeanza kambi rasmi leo katika ukumbi wa Harbous Klab kwa ajili ya kujiandaa na sherehe za Mei mosi zitakazofanyika katika ukumbi wa Urafiki Club, Dar es Salaam.

Kundi hilo ambalo sambamba na kutoa burudani hiyo pia linajihusisha na kucheza sarakasi pamoja na Ngonjera litakaa kambi hiyo kwa muda wa wiki moja ili kuweza kujiimarisha.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa SF group Camponies ltd ambayo ndio inasinamia kundi hilo Selina Koka alisema katika kambi hiyo watakuwa wakifanya mazoezi katika burudani zote wanazozitoa.

"kundi hili huwa linatoa burudani katika shughuli mbalimbali za kiserikali na hii ni moja ya shughuli za kiserikali na ndio maana tumeamua kuweza kambi ili kuweza kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya kusheherekea siku hiyo," alisema.

Aliongeza kuwa kundi hilo ambalo linajumla ya wanamuziki 22 linatarajia kuanza kutoa burudani kwa kila wiki katika ukumbi tofauti kama zilivyobendi nyingine ili kuweza kutoa burudani zaidi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Phabbian Salvatory 'Super Phabby' alisema wanaliandaa kundi hilo kutoa upinzani kwa bendi nyingine kongwe kama Extra bongo, Twanga na nyinginezo ili kuweza kujiweka katika ramani nzuri ya muziki wa dansi hapa nchini.

"hatutaki kuishia hapa tunataka kuwa kama bendi nyingine na hata tuwashinde kwa kuwapa upinzani mkubwa ili kuweza kuwaonyesha uwezo wetu tulionao," alisema.

Saturday, April 14, 2012

* Tomasi Mashari amchakaza Galile kwa pointi na kunyakua Ubingwa




Bondia SELEMANI GALILE akipambanma na THOMAS MASHARI 'Simba' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa uliofanyika Dar es Salaam MASHARI alishinda kwa pointi na kunyakua ubingwa.

Friday, April 13, 2012

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Mabalozi wa nchi tofauti

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Italy JAMES ALEX MSEKELA aliyefika ya Ikulu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dakta ALI SHEIN akifuatana na Balozi wa Uturuki hapa nchini ALI DAVUTOGLU aliyefika Ikulu ya mjini Zanzibar kufanya mazungumzo na Dakta SHEIN.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dakta ALI SHEIN akisalimiana na Balozi wa Burundi hapa nchini ISSA NTAMBUKA aliyefika Ikulu ya Zanzibar kuonana na Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi.

Tuesday, April 10, 2012

* Mwana-Filamu STEVEN KANUMBA azikwa Makaburi ya Kinondoni,mamia Wapoteza fahamu wakati wa Kuuaga Mwili wake


Watoto waliowahi kuigiza na marehemu STEVEN KANUMBA na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya KANUMBA.

Mama wa Marehemu STEVEN KANUMBA akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake.



Waombolezaji wa msiba wa Marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

KANUMBA atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.



Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.



Gari lililobeba mwili wa marehemu KANUMBA linaondoka katika viwanja vya Leaders kwenda Makaburi ya Kinondoni huku likiwa limezungukwa na waombolezaji.

(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)

Sunday, April 8, 2012

* Kanumba kuzikwa Makaburi ya Kinondoni Mama mzazi Atoa Msimamo

Hayati STEVEN KANUMBA
Masaa machache baada ya mama mzazi wa Kanumba kufika Jijini Dar es Salaam akitokea kwao Bukoba amekubaliana na maombi ya wapenzi wa mwanae na wana-bongo MOVIE kwamba mwanae azikwe hapa hapa DSM.

Hivyo Kanumba atazikwa makaburi ya kinondoni na ataagwa siku ya jumanne katika viwanja vya LEADERS Kinondoni.



Maneno ya Mwisho ya STEVEN CHARLES KANUMBA

* Rais Jakaya Kikwete atoa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Steven Kanumba

Rais Kikwete amefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba eneo la Sinza, Dar es Salaam, ambako amejiunga na mamia kwa mamia ya waombolezaji, wasanii na wana-familia kuombeleza kifo cha mmoja wa wasanii vijana, hodari zaidi na wenye vipaji vikubwa zaidi katika tasnia ya sanaa.

Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Kanumba, Rais Kikwete  ametia saini kitabu cha maombolezo na baadaye kuingia ndani kuzungumza kwa ufupi sana na wana-familia pamoja na wasanii wengi wa kike wa Tanzania.

Katika salamu zake za rambirambi kwa wanafamilia, Rais Kikwete amesema kwa kifupi tu: “Nimekuja kuhani msiba wa kijana wetu Steven Kanumba. Tulifahamiana sana wakati wa enzi ya uhai wake na mwaka jana nilimwalika Dodoma kwa ajili ya chakula cha mchana na wasanii wenzake wachache.

Ametutoka akiwa bado kijana sana lakini Mwenyezi Mungu ana mapenzi na uwezo wake. Nawaombeni kuweni na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba.”

Rais Kikwete pia amewaasa wasanii kuwasikiliza wana-familia katika maamuzi yote yanayohusiana na wapi azikwe marehemu. Marehemu Steven Charles Kanumba aliaga dunia usiku wa kuamkia jana, Jumamosi, Aprili 7, 2012. Alikuwa na umri wa miaka 28.

Hayati STEVEN CHARLES KANUMBA 'Mcheza Filamu'




Rais JAKAYA KIKWETE akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.



Rais KIKWETE akiongea na wanakamati ya msiba wa marehemu STEVEN KANUMBA Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam alikofika kuomboleza nao kifo hicho.

Friday, April 6, 2012

* Majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba yatangazwa




Rais JAKAYA KIKWETE akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo.

Wakishuhudia ni Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF IDDI Pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Mama CELINA KOMBANI.


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsubiri Rais KIKWETE kuja kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais KIKWETE akitoa ufafanuzi kuhusu Tume ya mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza, akisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa kwa mujibu sheria tume hiyo inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18.


   TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,

Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7

______________________________



UONGOZI WA JUU

1.Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA
- Mwenyekiti

2.Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI
- Makamu Mwenyekiti


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA

1.Prof. Mwesiga L. BAREGU


2.Nd. Riziki Shahari MNGWALI


3.Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI


4.Nd. Richard Shadrack LYIMO


5.Nd. John J. NKOLO


6.Alhaj Said EL- MAAMRY


7.Nd. Jesca Sydney MKUCHU


8.Prof. Palamagamba J. KABUDI


9.Nd. Humphrey POLEPOLE


10.Nd. Yahya MSULWA


11.Nd. Esther P. MKWIZU


12.Nd. Maria Malingumu KASHONDA


13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)


14.Nd. Mwantumu Jasmine MALALE


15.Nd. Joseph BUTIKU


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR


1.Dkt. Salim Ahmed SALIM


2.Nd. Fatma Said ALI


3.Nd. Omar Sheha MUSSA


4.Mhe. Raya Suleiman HAMAD


5.Nd. Awadh Ali SAID

6.Nd. Ussi Khamis HAJI


7.Nd. Salma MAOULIDI


8.Nd. Nassor Khamis MOHAMMED


9.Nd. Simai Mohamed SAID


10.Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA


11.Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN


12.Nd. Suleiman Omar ALI


13.Nd. Salama Kombo AHMED


14.Nd. Abubakar Mohammed ALI


15.Nd. Ally Abdullah Ally SALEH


UONGOZI WA SEKRETARIETI

1.Nd. Assaa Ahmad RASHID
- Katibu

2.Nd. Casmir Sumba KYUKI
- Naibu Katibu