Thursday, April 26, 2012

* Kichanga chaokotwa kitongoji cha Isevya Mkoani Tabora

Kichanga kikiwa kimetupwa na mtu ambae mpaka sasa bado hajafahamika eneo la Isevya mkoani Tabora.


Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora wakijadiliana Jambo kuhusu Tukio hilo. 

Dampo ambalo kitoto hicho kichanga kilitupwa , pembeni ni Baadhi ya wananchi pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi wakipata maelezo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.



Umati wa Wananchi wa eneo la Isevya Mkoani Tabora wakishuhudia tukio hilo la kutupwa kwa Kichanga.


Na Mwandishi wetu

Mtu asiyejulikana amekitupa kitoto kichanga kwenye dampo lililopo kwenye Soko la kata ya Isevya manispaa ya Tabora

Kichanga hicho  kinachokadiriwa kuwa na umri kati ya miezi nane na tisa kimeokotwa na mtu anayedaiwa kuwa na magonjwa ya akili ambaye alikwenda kutupa takataka katika dampo hilo na kukikuta kichanga hicho kikiwa kimefunikwa na khanga.

Hata hivyo mtu huyo anayefahamika soko la Isevya kwa kazi ya kubeba takataka,baada ya kugundua kichanga hicho kilichotapakaa damu nyingi alikichukua na kukipeleka sokoni hapo huku akilalamikia kitendo cha kutupwa kichanga hicho ambacho hakikuwa na uhai.

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Isevya walistaajabu tukio hilo huku zikiwashangaza zaidi kauli za mtu huyo ambaye huwa wakimfahamu kwa mapungufu ya akili.

Kwa upande mwingine maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho huku wakiwaomba wananchi kutoa taarifa za mtu atakayebainika kuwa amehusika na tukio hilo la kinyama.
 
Hata hivyo katika kata ya Isevya matukio utoaji mimba na kutupa watoto yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ingawa mara nyingi wanaojihusisha na matendo hayo wamekuwa wakifichwa.

No comments:

Post a Comment