Friday, February 24, 2012

Washiriki wa Halaiki ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar wakutana na Rais Shein




Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF ALI IDDI wakati wa hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.



Watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa wamevalia sare, wakisubiri kuanza kwa shughuli hiyo ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN.

Thursday, February 23, 2012

* Tanzania yasaini mkataba wa kupeleka washtakiwa wa Uharamia wa Ki-Somali katika Jela Husika



Rais JAKAYA KIKWETE na Waziri wa masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa na Afrika na Mazingira wa Uingereza HENDRY BELLINGHAM wakishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu.

Tuesday, February 21, 2012

* Waziri wa Habari Dakta Emmanuel Nchimbi awapatanisha Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi


Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI na Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakipeana mikono ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili,huku wapatanishi wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt EMMANUEL NCHIMBI(kushoto) pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU (kulia) wakishuhudia.


Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao.


Mkurugenzi wa Clouds Media Group RUGE MUTAHABA (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili.

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal aendelea na ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa


Makamu wa Rais wa Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ASHA BILAL wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi.


Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, GEORGE MBAULA (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chief wa Kabila hilo.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akitembelea shamba la ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa.



Makamu wa rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, EXAVERY KAYANZA PINDA, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi.

Sunday, February 19, 2012

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal akutana na mtafiti wa Masokwe hapa nchini


Makamu wa Rais  Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akipokea zawadi ya kitabu cha mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, JANE GOODALL aliyefika Ikulu ndogo ya Wlaya ya Mpanda mkoa wa Katavi kwa ajili ya mazungumzo.

JANE amekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti katika mapori ya Gombe na Mahale yaliyopo mkoa wa Kigoma na Katavi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL na mkewe Mama ASHA BILAL wakizungumza na Mtafiti bingwa wa Masokwe Duniani JANE GOODALL.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akielekezwa na mtafiti bingwa Duniani wa Masokwe, JANE GOODALL kuhusu ishara anazozitumia kuwasiliana na Masokwe na jinsi ya kuzungumza nao, wakati alipofika Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Saturday, February 18, 2012

* Rais Jakaya Kikwete aongoza matembezi ya Hisani yaliyoandaliwa na VODACOM Tanzania pamoja na Hospitali ya CCBRT


Rais JAKAYA KIKWETE akiongoza matembezi ya Hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya akina mama ya Baobab iliyo chini ya CCBRT jijini Dar es salaam.

Katika picha kutoka kulia Meya wa Ilala JERRY SLAA, Meya wa Kinondoni Bwana MWENDA, Bwana ERWIN TELEMANS Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, RENE MEZA Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bwana WILBROAD SLAA na kulia kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dakta HADJI MPONDA na Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Bwana ANDREW DUNNET pamoja na MWAMVITA MAKAMBA wa Vodacom Tanzania wakiwa katika matembezi hayo.



Rais JAKAYA KIKWETE akishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuongoza matembezi ya hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya akina mama wenye matatizo mbalimbali ya uzazi katika hospitali ya CCBRT.

Matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa Find your Moyo.

Friday, February 17, 2012

* Khitma ya Marehemu Tambaza Mohammed Tambaza kufanyika Jumamosi February 18, 2012 Dar es Salaam

Marehemu Tambaza Mohammed Tambaza

Kamati ya msiba wa ndugu yetu marehemu TAMBAZA MOHAMMED TAMBAZA inaarifu kwamba Khitma ya marehemu itasomwa Jumamosi hii February 18 mtaa wa Congo mwisho Kariakoo Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 6 mchana.

Marehemu TAMBAZA ambae alikuwa ni mwanamichezo na mwanaharakati wa maendeleo ya Jamii atakumbukwa kama mmoja wa wana-Dar es Salaam waliojizolea umaarufu mkubwa katika Jamii kutokana na Juhudi zake za kuwa mstari wa mbele katika kluendeleza mstakabali wa maendeleo ya wananchi.

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal aendelea na Ziara yake Mkoani Ruvuma


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji Makaa ya Mawe ya Tancoal, GRAEME ROBERTSON, wakati alipotembelea mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe unaoendelea eneo la Ruanda Wilaya ya Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Ruvuma.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akiweka Jiwe la Msingi katika mradi wa mashine za kuzalisha umeme Wilayani Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi mashine za kuzalisha umeme,Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tanesco, Injinia BONIFACE NJOMBE.

* Basi la kampuni ya Abood lapinduka likitokea Morogoro kuja Dar es Salaam


Wananchi wakitazama jinsi basi la ABOOD lilivyopinduka huku wengine wakiokoa abiria waliopo kwenye basi hilo asubuhi ya leo.


Basi la kampuni ya ABOOD likiwa limepinduka maeneo ya Mbezi likiwa linatoka Mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam asubuhi ya leo.

Chanzo cha ajali hii hakikujulikana ila inasemekana ni kutokana na dereve ku-overtake gari mbele na hatimaye kumshinda na kupinduka.

* Rais Jakaya Kikwete afungua mkutano wa mawaziri wa Kilimo kutoka nchi saba Barani Afrika



Rais JAKAYA KIKWETE akifungua mkutano wa Mawaziri wa Kilimo toka nchi saba za Afrika katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es salaam.


Rais JAKAYA KIKWETE akiongea na Mawaziri wa kilimo wa nchi saba za Afrika baada ya kufungua mkutano huo, Nyuma ya Rais KIKWETE ni kamishna wa Maendeleo vijijni na Kilimo wa Umoja wa Afrika Bi RHODA TUMUSSIME.

Thursday, February 16, 2012

* Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC yakutana na Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania NEC Jaji DAMIAN LUBUVA, akiongoza ujumbe wa Tume hiyo walipofika Ikuku Mjini Zanzibar kuonana na Rais, katikati Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, pia Makamo Mwenyekiti wa Tume hiyo HAMID MAHAMOUD HAMID.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akizungumza Ujumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, NEC ukiongozwa na Jaji DAMIAN LUBUVA (wa nne kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal atembelea mradi wa mto mkuju - Madini ya Urani



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Usalama Kazini, NASSOR ABDALLAH kuhusu vifaa vya usalama kazini vinavyotumika na wafanyakazi wa migodini wanapokuwa kazini, wakati Makamu wa Rais akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma alipotembelea mradi wa Mto Mkuju unaojiandaa na uchimbaji wa madini ya Urani kupitia kampuni yake ya Manta Tanzania Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, SAID MWAMBUNGU.

Wednesday, February 15, 2012

* Rais Kikwete atembelea kambi ya Ujasiriamali iliyopo katika kijiji cha Msoga mkoani Pwani




Rais JAKAYA KIKWETE akiwa katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha.

Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.

Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.

Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.

Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.

* Dakta Shein akutana na mwakilishi wa Shirika la Afya la Ulimwengu WHO Dakta Rufaro Chatora



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN, akizungumza na Dkt RUFARO R. CHATORA (WHO) Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni, nchini Tanzania, (kushoto) na Waziri wa Afya JUMA DUNI HAJI, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akifuatana na Dkt RUFARO R.CHATORA, (WHO) Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni, nchini Tanzania, (kushoto) na Waziri wa Afya JUMA DUNI HAJI , (kulia) baada ya mazungumzo yao Ikulu Mjini Zanzibar.

Monday, February 13, 2012

* Rais Jakaya Kikwete akutana na Mjumbe maalum kutoka Urusi




Rais JAKAYA KIKWETE akiagana na mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bwana MIKHAIL V. MARGELOV Ikulu jijini Dar es salaam.

Sunday, February 12, 2012

* Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM yakutana Mjini Dodoma


Mwenyekiti wa CCM Rais JAKAYA KIKWETE akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt MOHAMMED ALI SHEIN, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt AMANI ABEID KARUME, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj ALI HASSAN MWINYI, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) PIUS MSEKWA na Katibu Mkuu wa CCM  WILSOM MUKAMA kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu katika jengo la White House la Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma.



Sehemu ya wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika mkutano huo.

Friday, February 10, 2012

* Rais wa Zanzibar Dakta Ali Shein akutana na Balozi wa Sudan hapa nchini


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ALI  MOHAMMED SHEIN akisalimiana na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania Dkt YASSIR MOHAMMED ALI alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.



Rais wa Zanzibar Dkt ALI MOHAMMED SHEIN akizungumza na Balozi wa Sudan Nchini Tanzania Dkt YASSIR MOHAMMED ALI alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.