Thursday, June 14, 2012

* Waziri wa Habari Azungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Jijini Mwanza


Waziri wa Habari vijana, Utamaduni na Michezo Dakta FENELLA MUKANGARA akiongea na maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali jijini Mwanza.

Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na serikali kupitia vyombo vya habari.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo SETH KAMUHANDA mstari wa kwanza) akifuatilia mada  kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia  kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali ijini Mwanza.

Wengine wanaoonekana kwa nyuma ni maafisa habari na mawasiliano wa Serikali.


Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment