Wednesday, July 20, 2011

* Rais Jakaya Kikwete aanza Ziara ya Kihistoria nchini Afrika Kusini

Rais JAKAYA KIKWETE akiwa pamoja na Rais wa Afrika Kusini Bwana JACOB ZUMA
Rais JAKAYA KIKWETE amesema mataifa ya Afrika bado yanahitaji misaada ya Ki-maendeleo, ingawa wajibu wa kujiendeleza unabakia mikononi mwao na sio kwa mataifa ya Kigeni wakiwamo wafadhili.

Rais KIKWETE ambae yupo Afrika Kusini kwa ziara ya Kihistoria tangu taifa hilo lilipopata uhuru mwaka 1994, amewataka wafanyabiashara na wawekezaji nchini humo kuanzisha vitega uchumi na kuwekeza katika uchumi wa Tanzania kwa sababu ya vivutio vikubwa vilivyopo hapa nchini.

Amesema umefika wakati kwa Tanzania na Afrika Kusini kutumia uhusiano wa kihistoria ili kujenga mahusiano imara na ya karibu zaidi ya kiuchumi baina ya nchi hizo.

No comments:

Post a Comment