Friday, January 6, 2012

* Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal azindua Jengo jipya la makao makuu ya Polisi mkoa wa kusini Pemba



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akifunua Kitambaa ikiwa ni Ishara ya kuzindua rasmi Jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi lililopo eneo la Dunga, Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, MUSSA ALI MUSSA wakati akimuelekeza baadhi ya maeneo muhimu yaliyo ndani ya Jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya Polisi uliofanyika eneo la Dunga, Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

No comments:

Post a Comment