Monday, January 2, 2012

* Rais Jakaya Kikwete awaapisha makatibu wakuu wawili pamoja na naibu katibu mkuu mmoja Ikulu, Jijini Dar es Salaam



Picha tatu tofauti zikiwaonesha makatibu wakuu wawili pamoja na naibu katibu mkuu mmoja ambao wameapishwa na Rais JAKAYA KIKWETE katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, SUSAN PAUL, Katibu Mkuu Ikulu, PETER ALANAMBULA ILOMO na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ELIACKIM CHACHA, kabla ya kuapishwa na Rais JAKAYA KIKWETE.


Waziri wa Nishati na Madini, WILLIAM NGELLEJA, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ELIACKIM CHACHA, baada ya kuapishwa na Rais KIKWETE Ikulu  Jijini Dar es Salaam.


Rais JAKAYA KIKWETE,akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini WILLIAM NGELLEJA na Naibu wake,ADAM MALIMA,Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo.

No comments:

Post a Comment